Surah Tawbah aya 111 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ إِنَّ اللَّهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّهِ ۚ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴾
[ التوبة: 111]
Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa,
Surah At-Tawbah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Indeed, Allah has purchased from the believers their lives and their properties [in exchange] for that they will have Paradise. They fight in the cause of Allah, so they kill and are killed. [It is] a true promise [binding] upon Him in the Torah and the Gospel and the Qur'an. And who is truer to his covenant than Allah? So rejoice in your transaction which you have contracted. And it is that which is the great attainment.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qurani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa,.
Mwenyezi Mungu anatilia mkazo ahadi yake aliyo wapa Waumini wanao toa nafsi zao na mali yao kwa ajili ya Njia yake, kuwa hakika Yeye amenunua kwao hizo nafsi zao na mali yao kwa kuwalipa Pepo kuwa ndio thamani ya hivyo walivyo toa. Kwani wao wanapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Wanawauwa maadui wa Mwenyezi Mungu, au wao wanakufa mashahidi katika Njia yake. Na Mwenyezi Mungu amethibitisha ukweli huu katika Taurati na Injili, kama alivyo thibitisha katika Qurani. Wala hapana yeyote mwenye kumshinda Mwenyezi Mungu katika kutimiza ahadi. Basi furahini, enyi Waumini Mujaahidina, kwa biashara hii mlio uza nafsi zenu na mali yenu ambayo yatatoweka, na badala yake mkanunua Pepo itakayo baki milele. Na biashara hii ndio ushindi mkubwa kwenu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Wakasema: Wallahi! Mwenyezi Mungu amekufadhilisha wewe kuliko sisi, na hakika sisi tulikuwa wenye kukosa.
- Na hakika hutapata kiu humo wala hutapata joto.
- Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa
- Na anapo kuondosheeni madhara mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao Mlezi,
- Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao.
- Je! Nini wanangojea ila Saa iwajie kwa ghafla na wala wao hawatambui?
- Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli.
- Ni kama mfano wa Shetani anapo mwambia mtu: Kufuru. Na akikufuru humwambia: Mimi si pamoja
- Na tuliwapa ishara zetu, nao wakazipuuza.
- Je! Hazikukufikieni khabari za walio kabla yenu? Kaumu ya Nuhu, na A'adi, na Thamud, na
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Tawbah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Tawbah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Tawbah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers