Surah Tawbah aya 117 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿لَّقَد تَّابَ اللَّهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ مِن بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّهُ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴾
[ التوبة: 117]
Mwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya Nabii na Wahajiri na Ansari walio mfuata katika saa ya dhiki, pale baada ya kukaribia nyoyo za baadhi yao kugeuka. Basi akapokea toba yao, kwani hakika Yeye kwao wao ni Mpole na ni Mwenye kuwarehemu.
Surah At-Tawbah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Allah has already forgiven the Prophet and the Muhajireen and the Ansar who followed him in the hour of difficulty after the hearts of a party of them had almost inclined [to doubt], and then He forgave them. Indeed, He was to them Kind and Merciful.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Mwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya Nabii na Wahajiri na Ansari walio mfuata katika saa ya dhiki, pale baada ya kukaribia nyoyo za baadhi yao kugeuka. Basi akapokea toba yao, kwani hakika Yeye kwao wao ni Mpole na ni Mwenye kuwarehemu.
Mwenyezi Mungu Subhanahu amemfadhili Nabii wake na Masahaba wake wenye kuamini, walio wakweli, miongoni mwa Wahajiri na Ansari, walio toka pamoja naye kwenda pigana Jihadi wakati wa shida. (katika vita vya Tabuk) . Aliwaweka imara na akawalinda wasikhitalifiane, baada ya shida ya dhiki ya kuwafarikisha baina yao, hata zikakaribia nyoyo zao kuelekea kutaka kubaki nyuma wasitoke kwenda kwenye Jihadi. Tena Mwenyezi Mungu aliwasamehe kwa ile raghba yao iliyo wapitia ndani ya nafsi zao. Hakika Yeye Subhanahu ni Mwenye upole mwingi, na Mwenye rehema kubwa. Vita hivi vilikuwa mwezi wa Rajab mwaka wa 9 wa Hijra, baina ya Waislamu na Warumi. Na huitwa -Vita vya Dhiki-, Ghazwatu Usr, kwa sababu ya dhiki ya Waislamu waliyo kuwa nayo kwa ukosefu wa mali na zana. Katika vita hivi alijitolea Othman kulizatiti jeshi zima.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini.
- Na ndugu yangu Harun ni fasihi zaidi ulimi wake kuliko mimi. Basi mtume ende nami
- Huu ni Ukumbusho wa rehema ya Mola wako Mlezi kwa mja wake, Zakariya.
- Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho.
- Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Na kwa Mwenyezi Mungu yatarejeshwa mambo yote.
- Na Siku ya Kiyama utawaona walio msingizia uwongo Mwenyezi Mungu nyuso zao zimesawijika. Je! Si
- Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
- Na alipo elekea upande wa Madyana alisema: Asaa Mola wangu Mlezi akaniongoa njia iliyo sawa.
- Na wanaapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa kiapo chao ya kwamba ukiwaamrisha kwa yakini watatoka.
- Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Tawbah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Tawbah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Tawbah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers