Surah Tawbah aya 118 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَعَلَى الثَّلَاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا حَتَّىٰ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوا أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ اللَّهِ إِلَّا إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوا ۚ إِنَّ اللَّهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴾
[ التوبة: 118]
Na pia wale watatu walio achwa nyuma hata dunia wakaiona dhiki juu ya ukunjufu wake, na nafsi zao zikabanika, na wakayakinika kuwa hapana pa kumkimbia Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwake Yeye. Kisha akawaelekea kwa rehema yake ili nao waendelee kutubu. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu.
Surah At-Tawbah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And [He also forgave] the three who were left behind [and regretted their error] to the point that the earth closed in on them in spite of its vastness and their souls confined them and they were certain that there is no refuge from Allah except in Him. Then He turned to them so they could repent. Indeed, Allah is the Accepting of repentance, the Merciful.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na pia wale watatu walio achwa nyuma hata dunia wakaiona dhiki juu ya ukunjufu wake, na nafsi zao zikabanika, na wakayakinika kuwa hapana pa kumkimbia Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwake Yeye. Kisha akawaelekea kwa rehema yake ili nao waendelee kutubu. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu.
Na pia Mwenyezi Mungu aliwafadhili wale wanaume watatu walio baki nyuma wasitoke kwenda kwenye Jihadi katika vita vya Tabuk. Hawa hawakubaki nyuma kwa unaafiki. Ilikuwa inatarajiwa Mwenyezi Mungu atoe bayana ya hukumu yao. Ilivyo kuwa toba yao ni ya kweli, na majuto yao makubwa hata wakaiona dunia nyembamba juu ya upana wake, na nafsi zao zikaingiwa na dhiki kwa hamu na huzuni, na wakajua kuwa hapana pa kuikimbia ghadhabu ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa kumwomba Yeye msamaha na kurejea kwake. Hapo basi Mwenyezi Mungu aliwaongoa watubu. Na Yeye akawasamehe, ili wapate kuendelea na hali ya toba. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba za wenye kutubu, ni Mwingi wa kuwarehemu waja wake.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na Musa alipo omba maji kwa ajili ya watu wake, tulimwambia: Lipige jiwe kwa fimbo
- Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu?
- Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na akakupeni sura, na akazifanya nzuri sura zenu. Na
- Na Salamu juu ya Mitume.
- Na anaye tenda uovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akaomba maghfira kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta
- Hakika wale wafichao aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu, wakanunua kwacho thamani ndogo, hao hawali
- Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamzulii uwongo Mwenyezi Mungu.
- Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa
- Na lau Mwenyezi Mungu angeli penda, wasingeli shiriki. Na Sisi hatukukufanya wewe uwe mtunzaji wao.
- Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Tawbah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Tawbah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Tawbah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers