Surah Nahl aya 125 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ﴾
[ النحل: 125]
Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka.
Surah An-Nahl in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Invite to the way of your Lord with wisdom and good instruction, and argue with them in a way that is best. Indeed, your Lord is most knowing of who has strayed from His way, and He is most knowing of who is [rightly] guided.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka.
Ewe Nabii! Lingania, uwite watu kwenye Njia ya Haki ambayo Mola wako Mlezi amewataka watu wako waifuate. Na katika huo Wito wako pita njia ambayo inamnasibu kila mmoja wao. Waite wenye vyeo vya juu katika wao kwa maneno ya hikima kwa mujibu wa akili zao. Na watu wa kawaida walio baki kati yao walinganie kwa kuwapa mawaidha yanao waelekea, na kuwapigia mifano ya mambo wanayo pambana nayo ya kuwapeleka kwenye Haki, na uwaongoze kwenye njia fupi inayo wanasibu. Na jadiliana na watu wa dini zilizo tangulia katika watu wa Biblia, yaani Mayahudi na Wakristo, kwa kutumia hoja za kiakili, Mantiqi, na maneno laini, na majadiliano mazuri, si maneno ya ukali na matusi, ili uwakinaishe na uwavutie. Hii ndiyo njia ya Daawa (Wito), kuwaita watu kumwendea Mwenyezi Mungu -watu wa mila zote. Basi ifuate njia hii unapo waita, na baada ya hayo yaliyo baki mwachilie Mola wako Mlezi, ambaye anamjua aliye zama katika upotovu kati yao na akawa mbali na njia ya uwokovu, na nani ambaye aliye salimika, akaongoka, na akayaamini hayo uliyo waletea.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka
- Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na
- Bustani za milele wataziingia; iwe inapita kati yake mito. Humo watapata watakacho. Hivi ndivyo Mwenyezi
- Akasema: Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa sababu wananikanusha.
- Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa
- Na inapo kufikieni taabu katika bahari, hao mnao waomba wanapotea, isipo kuwa Yeye tu. Na
- Wakasema nao wamewakabili: Kwani mmepoteza nini?
- Je, wao wanayo miguu ya kwendea? Au wanayo mikono ya kutetea? Au wanayo macho ya
- Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa
- Na nipe waziri katika watu wangu,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nahl with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nahl mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nahl Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers