Surah Anam aya 157 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَوْ تَقُولُوا لَوْ أَنَّا أُنزِلَ عَلَيْنَا الْكِتَابُ لَكُنَّا أَهْدَىٰ مِنْهُمْ ۚ فَقَدْ جَاءَكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَذَّبَ بِآيَاتِ اللَّهِ وَصَدَفَ عَنْهَا ۗ سَنَجْزِي الَّذِينَ يَصْدِفُونَ عَنْ آيَاتِنَا سُوءَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يَصْدِفُونَ﴾
[ الأنعام: 157]
Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungeli kuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi imekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye kanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipa wanao jitenga na Ishara zetu adhabu kali kabisa kwa sababu ya kujitenga kwao.
Surah Al-Anam in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Or lest you say, "If only the Scripture had been revealed to us, we would have been better guided than they." So there has [now] come to you a clear evidence from your Lord and a guidance and mercy. Then who is more unjust than one who denies the verses of Allah and turns away from them? We will recompense those who turn away from Our verses with the worst of punishment for their having turned away.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungeli kuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi imekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye kanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipa wanao jitenga na Ishara zetu adhabu kali kabisa kwa sababu ya kujitenga kwao.
Na Sisi tumeiteremsha Qurani ili wasiseme pia: Lau kuwa sisi tumeteremshiwa ufunuo kama walivyo teremshiwa wao, tungeli washinda kwa uwongofu, na hali yetu ingeli kuwa bora zaidi, kwa sababu ya akili zetu ni pana zaidi na sisi tumetengenea vizuri! Baada ya hii leo hamna hoja ya kuasi kwenu. Wala hapana udhuru wa kauli yenu hii. Kwani Qurani imekujieni kutoka kwa Mola Mlezi wenu, nayo ni alama iliyo wazi ya ukweli wa Muhammad. Inabainisha yote mnayo yahitajia katika Dini yenu na dunia yenu. Inakuongoeni kwenye Njia iliyo sawa, na rehema kwenu kuifuata. Na hapana mwenye kudhulumu zaidi kuliko huyo anaye zikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu alizo ziteremsha katika Vitabu vyake, na Ishara zake alizo ziumba katika ulimwengu, naye akazipuuza na asiziamini, na wala asizitende! Na Sisi tutawaadhibu hao wanao zikataa Ishara zetu, wala hawazingatii adhabu yenye mwisho wa uchungu, kwa sababu ya kukataa kwao na kuacha kuzingatia kwao.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba.
- Alif Lam Mim (A. L. M.)
- Naye ndiye aliye zipeleka bahari mbili, hii tamu mno, na hii ya chumvi chungu. Na
- Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa
- Basi tembeeni katika nchi miezi mine, na jueni kwamba nyinyi hamwezi kumshinda Mwenyezi Mung, na
- Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza
- Na tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi tunasema kweli.
- Basi ubaya wa waliyo yatenda utawadhihirikia, na yatawazunguka waliyo yafanyia maskhara.
- Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini.
- Naye atakuja ridhika!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anam with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anam mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anam Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



