Surah Hud aya 88 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَرَزَقَنِي مِنْهُ رِزْقًا حَسَنًا ۚ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أُخَالِفَكُمْ إِلَىٰ مَا أَنْهَاكُمْ عَنْهُ ۚ إِنْ أُرِيدُ إِلَّا الْإِصْلَاحَ مَا اسْتَطَعْتُ ۚ وَمَا تَوْفِيقِي إِلَّا بِاللَّهِ ۚ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ﴾
[ هود: 88]
Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninayo dalili wazi inayo tokana na Mola wangu Mlezi, na ikawa Yeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Wala mimi sipendi kukukhalifuni nikafanya yale ninayo kukatazeni. Sitaki ila kutengeneza kiasi ninavyo weza. Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye naelekea.
Surah Hud in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
He said, "O my people, have you considered: if I am upon clear evidence from my Lord and He has provided me with a good provision from Him...? And I do not intend to differ from you in that which I have forbidden you; I only intend reform as much as I am able. And my success is not but through Allah. Upon him I have relied, and to Him I return.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninayo dalili wazi inayo tokana na Mola wangu Mlezi, na ikawa Yeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Wala mimi sipendi kukukhalifuni nikafanya yale ninayo kukatazeni. Sitaki ila kutengeneza kiasi ninavyo weza. Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye naelekea.
Yeye akasema: Enyi watu! Hebu nambieni, ikiwa mimi nina hoja iliyo wazi na ya yakini kutokana na Mola Mlezi wangu, naye akaniruzuku kwa fadhila yake riziki iliyo njema, je ingeli nifalia mimi nifiche aliyo niamrisha kukufikishieni, nako ni kuacha kuabudu masanamu, na kukutakeni mtimize vipimo na mizani, na muache kufanya uharibifu katika nchi? Na mimi si kama ninapenda kwenda kutenda haya ninayo kukatazeni, wala sitaki kwa mawaidha yangu, na nasaha zangu, na amri zangu, na makatazo yangu, ila kutengeneza kwa kadri ya ukomo wa uwezo wangu, na juhudi yangu, kama nilivyo jaaliwa. Wala sina uwezo wa kuifikilia haki ila kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kuungwa mkono naye, na ninamtegemea Yeye peke yake. Na kwake Yeye tu ndio ninarejea.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
- Na wale ambao wanapo kumbushwa Ishara za Mola wao Mlezi hawajifanyi viziwi nazo, na vipofu.
- Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu,
- Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni wanao msujudia.
- Atendaye ayatakayo.
- Na yaliyo kusibuni siku yalipo pambana majeshi mawili yalikuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na
- Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa.
- Msiwadhanie walio kufuru kwamba watashinda katika nchi. Na makaazi yao ni Motoni, na hakika ni
- Na wanamfanyia Mwenyezi Mungu ati ana mabinti, Subhanahu, Aliye takasika! Na wao wenyewe, ati ndio
- Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Hud with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Hud mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Hud Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers