Surah Muminun aya 18 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً بِقَدَرٍ فَأَسْكَنَّاهُ فِي الْأَرْضِ ۖ وَإِنَّا عَلَىٰ ذَهَابٍ بِهِ لَقَادِرُونَ﴾
[ المؤمنون: 18]
Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na tukayatuliza katika ardhi. Na hakika Sisi tunaweza kuyaondoa.
Surah Al-Muminun in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And We have sent down rain from the sky in a measured amount and settled it in the earth. And indeed, We are Able to take it away.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na tukayatuliza katika ardhi. Na hakika Sisi tunaweza kuyaondoa.
Na Sisi tumeteremsha kutoka mbinguni mvua kwa hikima na kipimo katika umbo lake na kuteremka kwake. Na kusahilisha kwa ajili ya manufaa tumeijaalia ikae juu ya uso wa ardhi na ndani yake chini. Na Sisi hakika ni wenye kuweza kuiondoa wasipate kunafiika nayo. Lakini hatukufanya hayo kwa kukuoneeni huruma. Basi muaminini Mwenye kuiumba na mumshukuru. -Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na tukayatuliza katika ardhi. Na hakika Sisi tunaweza kuyaondoa.- Aya hii tukufu inaashiria maana ya kisayansi yenye kukhusu mzunguko wa maji katika ardhi. Yajuulikana kuwa mvuke unao paa kutoka baharini hupelekea kufanyika mawingu ambayo ndiyo huteremsha mvua. Na hivyo ndio chanzo cha maji matamu juu ya uso wa ardhi, na ndio chombo cha msingi cha uhai wa ardhini. Kutokana na mvua ndio huzuka mito inayo zua uhai katika sehemu kamwe zisio pitikiwa na mvua. Kisha hiyo mito inamiminika baharini, na khulka inarejea tena kutoka baharini kwenda angani na kwendea nchi kavu, na kisha kuingia baharini mara ya pili. Isipo kuwa baadhi ya hayo maji ya mvua yanatulia na yanazama kuhifadhika katika mahodhi ya chini ya ardhi, yakawekeka kwa muda mrefu. Mfano wa hayo ni hayo maji yanayo patikana chini ya Jangwa la Magharibi katika Libya, ambayo yamegunduliwa na watafiti hivi karibuni kutokana na asli yake ya kale. Na huenda maji kama haya yalio hifadhika chini yakapatwa na mabadiliko ya joto wanayo yaita wataalamu wa ilimu ya tabaka za ardhi (Geology) kuwa ni Mikondo ya Jiolojia, ikenda hiyo na maji mpaka pahala pengine pakavu, ikaleta uhai baada ya kuwa ni maiti. Na Aya hii inaonyesha hikima kubwa ya uenezaji wa maji kwa kipimo, yaani kipimo cha haki na hikima, kwa ajili ya kuleta manufaa na kupinga madhara. Na tena maana nyengine ya Aya tukufu ni kufahamisha apendavyo Mwenye Kuumba, Aliye tukuka, navyo ni kujaalia yawepo maji ya kiasi maalumu katika bahari za ulimwengu kutosha kuwepo mizani ya joto la kufaa katika sayari hii, na ili isiwepo khitilafu kubwa mno baina ya joto la siku za joto, na baridi ya siku za baridi, hata ikawa ni muhali kubakia uhai, kama ilivyo katika sayari nyengine na katika mwezi. Kadhaalika maji ya ardhi yanateremka kwa kiasi maalumu, hayazidi yakafunika ardhi yote, wala hayatindikii sana hata yasipatikane hata kidogo kunyweshea baadhi ya nchi kavu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hawawezi watu wowote kuitangulia ajali yao, wala kuchelewa.
- Huyu si lolote ila ni mtu anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, wala sisi sio wa
- Ikawa inakwenda nao katika mawimbi kama milima. Na Nuhu akamwita mwanawe naye alikuwa mbali: Ewe
- Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
- Jueni kuwa hakika ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na ardhini. Hakika Yeye anajua mlio
- Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera.
- Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi.
- Na pale Mola wako Mlezi alipo waleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na
- Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake walio deka kwa starehe walisema:
- Na wanapo ambiwa: Kateremsha nini Mola wenu Mlezi? Husema: Hadithi za kubuni za watu wa
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Muminun with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Muminun mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Muminun Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers