Surah Nisa aya 19 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُوا النِّسَاءَ كَرْهًا ۖ وَلَا تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُوا بِبَعْضِ مَا آتَيْتُمُوهُنَّ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا﴾
[ النساء: 19]
Enyi mlio amini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu. Wala msiwadhikishe ili mwapokonye baadhi ya mlivyo wapa - isipo kuwa wakifanya uchafu ulio wazi. Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
O you who have believed, it is not lawful for you to inherit women by compulsion. And do not make difficulties for them in order to take [back] part of what you gave them unless they commit a clear immorality. And live with them in kindness. For if you dislike them - perhaps you dislike a thing and Allah makes therein much good.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Enyi mlio amini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu. Wala msiwadhikishe ili mwapokonye baadhi ya mlivyo wapa - isipo kuwa wakifanya uchafu ulio wazi. Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake.
Enyi mlio amini! Haikujuziini kuwafanya wanawake kama bidhaa, mkiwarithi wake zenu bila ya mahari na bila ya ridhaa yao. Wala msiwadhulumu kwa kuwadhikisha ili wapate kusamehe baadhi ya mahari mlio wapa. Wala msiwadhiki ili wapate kukurejesheeni mali mlio wapa, ila ikiwa wakifanya kosa wazi la kuwacha utiifu, au la tabia mbovu, au la ukahaba. Hapo mnaweza kuwadhikisha au kuchukua baadhi ya mlicho wapa wakati wa kufarikiana nao. Na ni waajibu wenu, enyi Waumini, kukaa na wake zenu kwa vizuri, kwa maneno mema na vitendo vyema. Ikiwa mtawachukia kwa aibu fulani katika tabia au katika umbo au mengineyo, basi juu ya hivyo subirini. Msifanye haraka kuwaacha, kwani asaa Mwenyezi Mungu akajaalia kheri nyingi katika hicho hicho mkichukiacho. Na ujuzi wa mambo yote uko kwa Mwenyezi Mungu tu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?
- Basi tulipo waondolea adhabu hiyo, mara wakaingia kuvunja ahadi.
- Na zitadhalilika nyuso mbele ya Aliye Hai Milele, Mwangalizi Mkuu. Na atakuwa ameharibikiwa mwenye kubeba
- Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
- Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.
- Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anaye zuilia mbingu na ardhi zisiondoke. Na zikiondoka hapana yeyote wa
- Na wachache katika wa mwisho.
- Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu
- Masihi mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume. Wamekwisha pita Mitume kabla yake. Na
- Enyi mlio kufuru! Msilete udhuru leo. Hakika mnalipwa mliyo kuwa mkiyatenda.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers