Surah Baqarah aya 231 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ سَرِّحُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ ۚ وَلَا تُمْسِكُوهُنَّ ضِرَارًا لِّتَعْتَدُوا ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ وَلَا تَتَّخِذُوا آيَاتِ اللَّهِ هُزُوًا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ وَمَا أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّنَ الْكِتَابِ وَالْحِكْمَةِ يَعِظُكُم بِهِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴾
[ البقرة: 231]
Na mtakapo wapa wanawake t'alaka, nao wakafikia kumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema au waachilieni kwa wema. Wala msiwarejee kwa kuwadhuru mkafanya uadui. Na atakaye fanya hivyo, amejidhulumu nafsi yake. Wala msizichukulie Aya za Mwenyezi Mungu kwa maskhara. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, na aliyo kuteremshieni katika Kitabu na hikima anacho kuonyeni kwacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And when you divorce women and they have [nearly] fulfilled their term, either retain them according to acceptable terms or release them according to acceptable terms, and do not keep them, intending harm, to transgress [against them]. And whoever does that has certainly wronged himself. And do not take the verses of Allah in jest. And remember the favor of Allah upon you and what has been revealed to you of the Book and wisdom by which He instructs you. And fear Allah and know that Allah is Knowing of all things.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na mtakapo wapa wanawake talaka, nao wakafikia kumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema au waachilieni kwa wema. Wala msiwarejee kwa kuwadhuru mkafanya uadui. Na atakaye fanya hivyo, amejidhulumu nafsi yake. Wala msizichukulie Aya za Mwenyezi Mungu kwa maskhara. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, na aliyo kuteremshieni katika Kitabu na hikima anacho kuonyeni kwacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Mnapo wawacha wake wakakaribia kumaliza eda zao mnaweza kuwarejea kwa makusudio ya uadilifu na kukaa nao kwa wema bila ya kuwadhuru, na pia mnaweza kuwaacha watimize eda zao kwa kuzingatia muamala mwema ulio laiki wakati wa kufarikiana bila ya kuwatendea mabaya. Wala haijuzu katika kuwarejea ikawa makusudio yake ni madhara na kuirefusha eda. Mwenye kutenda hayo basi mwenyewe amejinyima starehe ya maisha ya mke na mume, na imani ya watu kwake, na anastahiki kukasirikiwa na Mwenyezi Mungu. Wala msizifanyie maskhara na mchezo na kuwa ni upuuzi hukumu za Mwenyezi Mungu zilizo kuja katika Aya hizi kwa ajili ya kutengeza maisha ya kinyumba, na zikaweka khatamu za ukoo katika mikono ya wakili, naye ni mume, mkawa mnatoa talaka bila ya sababu, na mkawapatisha wake zenu madhara na maudhi. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu kwa kukupangieni mpango bora kabisa katika maisha ya ndoa, na pia kwa aliyo kuteremshieni katika Kitabu kilicho bainisha wazi ujumbe wa Muhammad, na ilimu mbali mbali zenye manufaa, na mifano na hadithi za kukuwaidhini na kukuongoeni. Na jikingeni na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Jueni kuwa Mwenyezi Mungu anajua siri zenu na mnayo dhihirisha na niya zenu na vitendo vyenu. Naye ni Mwenye kukulipeni kwa myatendayo.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Nyinyi - ulipo kusibuni msiba ambao nyinyi mmekwisha watia mara mbili mfano wa huo -
- Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye.
- Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji Mjuzi.
- Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake
- Na akamwona mara nyingine,
- Anaye kadhibisha na kupa mgongo.
- Na hawatoacha kuwamo humo.
- Sema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Kila umma una muda
- Na wanapo panda katika marikebu, humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafia ut'iifu. Lakini anapo wavua wakafika
- Basi jicho litapo dawaa,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



