Surah Baqarah aya 260 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ أَرِنِي كَيْفَ تُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِن ۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَٰكِن لِّيَطْمَئِنَّ قَلْبِي ۖ قَالَ فَخُذْ أَرْبَعَةً مِّنَ الطَّيْرِ فَصُرْهُنَّ إِلَيْكَ ثُمَّ اجْعَلْ عَلَىٰ كُلِّ جَبَلٍ مِّنْهُنَّ جُزْءًا ثُمَّ ادْعُهُنَّ يَأْتِينَكَ سَعْيًا ۚ وَاعْلَمْ أَنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴾
[ البقرة: 260]
Na alipo sema Ibrahim: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe vipi unavyo fufua wafu. Mwenyezi Mungu akasema: Kwani huamini? Akasema: Hasha! Lakini ili moyo wangu utue. Akamwambia: Twaa ndege wane na uwazoeshe kwako, kisha uweke juu ya kila kilima sehemu, kisha wete, watakujia mbio. Na ujue kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, na Mwenye hikima.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And [mention] when Abraham said, "My Lord, show me how You give life to the dead." [Allah] said, "Have you not believed?" He said, "Yes, but [I ask] only that my heart may be satisfied." [Allah] said, "Take four birds and commit them to yourself. Then [after slaughtering them] put on each hill a portion of them; then call them - they will come [flying] to you in haste. And know that Allah is Exalted in Might and Wise."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na alipo sema Ibrahim: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe vipi unavyo fufua wafu. Mwenyezi Mungu akasema: Kwani huamini? Akasema: Hasha! Lakini ili moyo wangu utue. Akamwambia: Twaa ndege wane na uwazoeshe kwako, kisha uweke juu ya kila kilima sehemu, kisha wete, watakujia mbio. Na ujue kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, na Mwenye hikima.
Kitaje pia kisa cha Ibrahim alipo sema: Mola wangu Mlezi nionyeshe vipi unahuisha maiti. Mola wake Mlezi akamuuliza Ibrahim, juu ya imani yake kuamini kufufuliwa wafu, ili ajibu Ibrahim kuondoa shaka kabisa katika imani yake. Mwenyezi Mungu akamwambia: Kwani huamini kufufuliwa wafu? Ibrahim akajibu: Mimi naamini, lakini nimetaka ili moyo uzidi kutua. Akasema Mwenyezi Mungu: Basi wachukue ndege wane uwe nao ili uwajue vilivyo. Kisha uwagawe baada ya kuwachinja, na juu ya kila kilima katika vilima vilio jirani weka sehemu yao. Kisha uwete, watakujia mbio, nao ni wahai kama walivyo kuwa. Na jua kuwa Mwenyezi Mungu hashindwi na lolote. Naye ni Mwenye hikima iliyo pita hadi katika kila kitu. Ametaja Al Fakhri Al Razi na wengineo kuwa yapo maoni mengine juu ya tafsiri ya maneno haya matukufu. Nayo ni kuwa Ibrahim hakuwachinja wale ndege, wala hakuamrishwa kuwachinja. Bali aliamrishwa awakusanye kwa kuwazoesha kukaa naye. Kisha akawagawa akaweka juu ya kila kilima ndege mmoja. Kisha akawaita wakamjia. Na hii ni namna Mwenyezi Mungu Mtukufu anavyo umba, ni kwa amri yake ya -Kuwa- basi huwa, kama alivyo waita wakaja
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Wala sisi hatutaadhibiwa.
- Anaye sikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, kisha anashikilia yale yale aliyo katazwa, na anajivuna,
- Mna nini hata hamsemi?
- Khabari za wakosefu:
- Na shika Sala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na
- Mtume anaye kusomeeni Aya za Mwenyezi Mungu zinazo bainisha, ili kuwatoa walio amini na wakatenda
- Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu.
- Ati wanawafanya viumbe kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu, nao hawaumbi, bali wao ndio wanaumbwa?
- Lakini tukiwaondolea adhabu mpaka muda fulani wao waufikie, mara wakivunja ahadi yao.
- Basi kuleni katika walio somewa jina la Mwenyezi Mungu, ikiwa mnaziamini Aya zake.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers