Surah Nisa aya 34 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّهُ ۚ وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا﴾
[ النساء: 34]
Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Men are in charge of women by [right of] what Allah has given one over the other and what they spend [for maintenance] from their wealth. So righteous women are devoutly obedient, guarding in [the husband's] absence what Allah would have them guard. But those [wives] from whom you fear arrogance - [first] advise them; [then if they persist], forsake them in bed; and [finally], strike them. But if they obey you [once more], seek no means against them. Indeed, Allah is ever Exalted and Grand.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika utiifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikutiini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu.
Wanaume wana haki ya kuwaangalia na kuwachunga wanawake, na kuwasimamia katika mambo yao kwa vile Mwenyezi Mungu amewapa wao wanaume sifa za kuweza kuisimamia haki hii, na kwa kuwa wao ndio wanao hangaika na kufanya juhudi ya kutafuta mali ya kuutumilia ukoo mzima. Basi wanawake wema wanakuwa ni watiifu kwa Mwenyezi Mungu na waume zao. Ni wenye kuhifadhi vyote ambavyo waume zao hawavioni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameamrisha vihifadhiwe, na kwa kuwapa wao tawfiki. Na wanawake wanao onyesha kuanza uasi wanasihini kwa maneno yenye kuathiri. Kama hawakusikia tenganeni nao kitandani. Hawakusikia, watieni adabu kwa pigo dogo, si la kuwajuruhi wala kuwadhalilisha. Wakirejea kwenye utiifu wenu kwa njia mojapo katika hizi tatu basi msiwatafutie kisababu cha kuwatesa zaidi kuliko haya. Hakika Mwenyezi Mungu yuko juu yenu, naye atakupatilizeni pindi mkiwaudhi wake zenu au mkawafanyia jeuri.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa.
- Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji?
- Na wanapo itwa kumuendea Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, kipo kikundi
- Hakika siku ya Sabato (Jumaamosi) waliwekewa wale walio khitalifiana kwa ajili yake. Na hakika Mola
- Hakika katika haya ipo Ishara, lakini si wengi wao walio kuwa Waumini.
- Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha?
- Na hakika tulikwisha kufanyia hisani mara nyengine...
- Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini?
- Wala hawana toba wale wafanyao maovu mpaka yakamfikia mmoja wao mauti, kisha hapo akasema: Hakika
- (Musa) akasema: Mola Mlezi wangu! Nisamehe mimi na ndugu yangu, na ututie katika rehema yako.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers