Surah Raad aya 4 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَفِي الْأَرْضِ قِطَعٌ مُّتَجَاوِرَاتٌ وَجَنَّاتٌ مِّنْ أَعْنَابٍ وَزَرْعٌ وَنَخِيلٌ صِنْوَانٌ وَغَيْرُ صِنْوَانٍ يُسْقَىٰ بِمَاءٍ وَاحِدٍ وَنُفَضِّلُ بَعْضَهَا عَلَىٰ بَعْضٍ فِي الْأُكُلِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴾
[ الرعد: 4]
Na katika ardhi vimo vipande vilivyo karibiana, na zipo bustani za mizabibu, na mimea mingine, na mitende yenye kuchipua kwenye shina moja na isio chipua kwenye shina moja, nayo inatiliwa maji yale yale. Na tunaifanya baadhi yao bora kuliko mengine katika kula. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanao tia mambo akilini.
Surah Ar-Rad in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And within the land are neighboring plots and gardens of grapevines and crops and palm trees, [growing] several from a root or otherwise, watered with one water; but We make some of them exceed others in [quality of] fruit. Indeed in that are signs for a people who reason.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na katika ardhi vimo vipande vilivyo karibiana, na zipo bustani za mizabibu, na mimea mingine, na mitende yenye kuchipua kwenye shina moja na isio chipua kwenye shina moja, nayo inatiliwa maji yale yale. Na tunaifanya baadhi yao bora kuliko mengine katika kula. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanao tia mambo akilini.
Na hakika hiyo ardhi nafsi yake ina maajabu. Ndani yake vipo vipande vilivyo karibiana, navyo juu ya hivyo vina udongo mbali mbali. Vingine ardhi yaabisi, na vingine vya rutba, ijapo kuwa ni udongo ule ule. Ndani yake yapo mabustani yaliyo jaa miti ya mizabibu, na ndani yake mazao mengine yanavunwa, na mitende yenye kuzaa, nayo ama iliyo kusanyika au iko mbali mbali. Na yote hayo ijapo kuwa inanyweshwa maji yale yale yanakhitalifiana kwa utamu wao. Na hakika katika ajabu hizi zipo dalili wazi za kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu kwa mwenye akili ya kufikiria. Aya hii tukufu inaonyesha ilimu ya ardhi (Geology) na ilimu ya mazingira (Ecology) na athari yao juu ya sifa za mimea. Inajuulikana katika ilimu kuwa rutuba ya ardhi inategemea juu ya chembe chembe za maadeni zinazo khitalifiana kwa namna na ukubwa, na maji yanayo toka kwenye mvua, na hewa, na vitu vyenye asili ya uhai, kama mimea na vyenginevyo, ambavyo hupatikana juu ya udongo au ndani yake. Huwapo hivyo kwa mamilioni vidogo vidogo hata havionekani kwa jicho tu. Kwa jumla ukizingatia haya utaona yanaonyesha uwezo wa Muumba na busara ya uumbaji, kwani ardhi kama wasemavyo wakulimu inakhitalifiana kila shubiri. Na inajuulikana kwa wanazuoni wa sayansi kuwa ukipatikana upungufu katika hivyo vitu vya msingi katika udongo basi hudhihirisha upungufu wake katika mimea, na kwa hivyo wakulima hujalizia upungufu huo kwa kutia mbolea mbali mbali na hutengeneza hali ya mazingira. Na hayo yana athari zake juu ya mazao ikiwa kwa mmea wa namna moja au namna mbali. Ametakasika Mwenyezi Mungu ambaye katika mikono yake upo ufalme wa kila kitu, naye ni Muweza wa kila kitu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Atakumbuka mwenye kuogopa.
- Na mkiwapa t'alaka kabla ya kuwagusa, na mmekwisha wawekea hayo mahari makhsusi, basi wapeni nusu
- Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote
- Na walio Motoni watawaambia walinzi wa Jahannamu: Mwombeni Mola wenu Mlezi atupunguzie walau siku moja
- Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na anaye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Yeye
- Haya haya tuliahidiwa sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni hadithi za uwongo
- Kwa kuyakataa tuliyo wapa. Basi stareheni. Mtakuja jua!
- Na tunaye mzeesha tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je! hawazingatii?
- Na haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwahisabu watu kuwa wamepotea baada ya kwisha waongoza mpaka awabainishie
- Hayo ni hivyo kwa sababu mlikuwa akiombwa Mwenyezi Mungu peke yake mnakataa. Na akishirikishwa mnaamini.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Raad with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Raad mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Raad Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers