Surah Raad aya 3 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَهُوَ الَّذِي مَدَّ الْأَرْضَ وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْهَارًا ۖ وَمِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ جَعَلَ فِيهَا زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ ۖ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴾
[ الرعد: 3]
Na ndiye aliye itandaza ardhi na akaweka humo milima na mito. Na katika kila matunda akafanya dume na jike. Huufunika usiku juu ya mchana. Hakika katika haya zimo Ishara kwa watu wanao fikiri.
Surah Ar-Rad in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And it is He who spread the earth and placed therein firmly set mountains and rivers; and from all of the fruits He made therein two mates; He causes the night to cover the day. Indeed in that are signs for a people who give thought.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na ndiye aliye itandaza ardhi na akaweka humo milima na mito. Na katika kila matunda akafanya dume na jike. Huufunika usiku juu ya mchana. Hakika katika haya zimo Ishara kwa watu wanao fikiri.
Na Subhanahu, Mwenyezi Mungu Aliye takasika, ndiye aliye kukunjulieni ardhi, akaidhalilisha ili muweze kutembea juu yake mashariki na magharibi. Na Yeye akajaalia katika hii ardhi milima iliyo simama imara, na mito ya maji matamu inayo miminika. Na akajaalia kwa hayo maji matunda ya kabila mbali mbali yanayo zaliana, na kati ya kabila hizo namna mbali mbali, mengine matamu na mengine makali, mengine meupe, na mengine meusi. Na Yeye Subhanahu huufunika mchana kwa usiku. Na hakika katika huu ulimwengu na ajabu zake zimo alama wazi za kuthibitisha uwezo wa Mwenyezi Mungu na Umoja wake kwa anaye fikiri akazingatia. Mwenyezi Mungu Mtukufu amejaalia katika kila mimea dume na jike ili ipate kupandishika sehemu ya uke kwa chembe za uzazi zilioko katika sehemu za ume. Na kwa hivyo ndio huzalikana namna kwa namna na kwa wingi.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hakika kuamka usiku kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno yake yanatua zaidi.
- Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza, mpaka wakiondoka kwako huwauliza walio pewa ilimu: Amesema nini
- Na walio kufuru wataongozwa kuendea Jahannamu kwa makundi. Mpaka watakapo ifikia itafunguliwa milango yake, na
- Ewe Nabii! Waambie mateka waliomo mikononi mwenu: Kama Mwenyezi akiona kheri yoyote nyoyoni mwenu atakupeni
- - Kama yaliyo wapata watu wa Firauni na wale walio kuwa kabla yao. Walikanusha Ishara
- Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni.
- Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau
- Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni!
- Waseme: Lakini nyinyi! Hamna mapokezi mazuri! Nyinyi ndio mlio tusabibisha haya, napo ni pahala paovu
- Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi? Hauwi mnong'ono
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Raad with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Raad mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Raad Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers