Surah An Nur aya 45 , Swahili translation of the meaning Ayah.

  1. Arabic
  2. tafsir
  3. mp3
  4. English
Quran in Swahili QUR,ANI TUKUFU na tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili - Ali Muhsen Alberwany & English - Sahih International : Surah An Nur aya 45 in arabic text(The Light).
  
   
ayat 45 from Surah An-Nur

﴿وَاللَّهُ خَلَقَ كُلَّ دَابَّةٍ مِّن مَّاءٍ ۖ فَمِنْهُم مَّن يَمْشِي عَلَىٰ بَطْنِهِ وَمِنْهُم مَّن يَمْشِي عَلَىٰ رِجْلَيْنِ وَمِنْهُم مَّن يَمْشِي عَلَىٰ أَرْبَعٍ ۚ يَخْلُقُ اللَّهُ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
[ النور: 45]

Na Mwenyezi Mungu ameumba kila kinyama kutokana na maji. Wengine katika wao huenda kwa matumbo yao, na wengine huenda kwa miguu miwili, na wengine huenda kwa miguu mine. Mwenyezi Mungu huumba ayatakayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Surah An-Nur in Swahili

Swahili Translation - Al-Barwani

English - Sahih International


Allah has created every [living] creature from water. And of them are those that move on their bellies, and of them are those that walk on two legs, and of them are those that walk on four. Allah creates what He wills. Indeed, Allah is over all things competent.


Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili


Na Mwenyezi Mungu ameumba kila kinyama kutokana na maji. Wengine katika wao huenda kwa matumbo yao, na wengine huenda kwa miguu miwili, na wengine huenda kwa miguu mine. Mwenyezi Mungu huumba ayatakayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.


Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na ndiye aliye anzisha kila kitu kwa kupenda kwake. Na akaumba kila kilicho hai kutokana na asili moja ya shirika, nayo ni maji. Na kwa hivyo kila kihai hakiachi kuwa na maji. Kisha zinawakhitalifisha khitilafu nyengine kwa namna, na uwezo, na sura, na kadhaalika. Katika wanyama wapo wanao tambaa kwa matumbo yao, kama samaki, na nyoka. Na wapo wanao kwenda kwa miguu miwili kama wanaadamu na ndege. Na wapo wanao kwenda kwa miguu mine kama mahayawani wengi wa kufugwa na wa mwituni. Mwenyezi Mungu huumba apendavyo kwa njia mbali mbali, kuonyesha uwezo wake na ujuzi wake. Kwani ni Mwenye kutaka atakacho, na Mwenye kukhitari apendacho. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu. -Na Mwenyezi Mungu ameumba kila kinyama kutokana na maji. Wengine katika wao huenda kwa matumbo yao, na wengine huenda kwa miguu miwili, na wengine huenda kwa miguu mine. Mwenyezi Mungu huumba ayatakayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.- Maji katika Aya hii tukufu ni maji ya uzazi, yaani vinyama vinavyo toa manii. Na Aya hii si kama imetangulia msafara wa sayansi katika kubainisha kuzalikana mtu kutokana na tone la manii, kama ilivyo kuja katika kauli yake Aliye tukuka: -Hebu naajitazame mtu, ameummbwa kwa kitu gani? Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa.- (Sura Attariq 5,6), bali imetangulia pia katika kubainisha kwamba kila kinyama kinacho kwenda kwenye ardhi kimeumbwa kwa njia ya kuzalikana na vinyama vya manii, na vinga khitalifiana hivyo vinyama vya manii na sifa zao katika kila namna mnamo hizo namna za vinyama. Katika maana za kisayansi ambazo zaweza kuwa nazo hii Aya ni kuwa maji ni msingi wa kila kiumbe kilicho hai. Kwa mfano mwili wa mtu umekusanya 70% ya uzito wake kuwa ni maji. Yaani mtu mwenye uzito wa kilo 70, kiasi kilo 50 ni maji. Na kabla ya kuteremka Qurani haya hayakuwa yakijuulikana kabisa ya kuwa mtu ana sehemu hii kubwa ya mwili wake kuwa ni maji. Na maji ndio chakula cha dharura kabisa kwa mwanaadamu. Kwani hali mtu yamkini aishi siku 60 bila ya kula chakula chochote, hawezi kuishi bila ya maji kwa zaidi kuliko siku 3 mpaka 10 mwisho wake. Na maji ndio msingi wa kufanyika damu, na maji ya limfo, na ya katika ubongo wa mifupa, vimwagavyo na mwili, kama mkojo, na jasho, na machozi, na mate, na nyongo, na maziwa, na maji yanayo patikana katika viungo, na ambayo ndiyo sababu ya ulaini wa mwili. Na yakikosekana 20% ya maji yake basi mwanaadamu hukabiliwa na mauti. Na maji huyayusha vyakula vikasahilika kufyonzeka. Na kadhaalika huyayusha makombo yenye asili ya vilivyo hai au maadini katika mkojo na jasho. Na kwa namna hii maji yana sehemu kubwa zaidi na muhimu kabisa katika kuumbwa kwa mwili. Na kwa hivyo yamkini kusema kwamba kila kiumbe kilicho hai kimeumbwa kutokana na maji.

English Türkçe Indonesia
Русский Français فارسی
تفسير Bengali Urdu

listen to Verse 45 from An Nur


Ayats from Quran in Swahili


Quran Surah in Swahili :

Al-Baqarah Al-'Imran An-Nisa'
Al-Ma'idah Yusuf Ibrahim
Al-Hijr Al-Kahf Maryam
Al-Hajj Al-Qasas Al-'Ankabut
As-Sajdah Ya Sin Ad-Dukhan
Al-Fath Al-Hujurat Qaf
An-Najm Ar-Rahman Al-Waqi'ah
Al-Hashr Al-Mulk Al-Haqqah
Al-Inshiqaq Al-A'la Al-Ghashiyah

Download Surah An Nur with the voice of the most famous Quran reciters :

Surah An Nur mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter An Nur Complete with high quality
Surah An Nur Ahmed El Agamy
Ahmed Al Ajmy
Surah An Nur Bandar Balila
Bandar Balila
Surah An Nur Khalid Al Jalil
Khalid Al Jalil
Surah An Nur Saad Al Ghamdi
Saad Al Ghamdi
Surah An Nur Saud Al Shuraim
Saud Al Shuraim
Surah An Nur Abdul Basit Abdul Samad
Abdul Basit
Surah An Nur Abdul Rashid Sufi
Abdul Rashid Sufi
Surah An Nur Abdullah Basfar
Abdullah Basfar
Surah An Nur Abdullah Awwad Al Juhani
Abdullah Al Juhani
Surah An Nur Fares Abbad
Fares Abbad
Surah An Nur Maher Al Muaiqly
Maher Al Muaiqly
Surah An Nur Muhammad Siddiq Al Minshawi
Al Minshawi
Surah An Nur Al Hosary
Al Hosary
Surah An Nur Al-afasi
Mishari Al-afasi
Surah An Nur Yasser Al Dosari
Yasser Al Dosari


Sunday, May 12, 2024

لا تنسنا من دعوة صالحة بظهر الغيب