Surah Al Imran aya 49 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَرَسُولًا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنِّي قَدْ جِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ أَنِّي أَخْلُقُ لَكُم مِّنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِ اللَّهِ ۖ وَأُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ وَأُحْيِي الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِ اللَّهِ ۖ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴾
[ آل عمران: 49]
Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi ni wenye kuamini.
Surah Al Imran in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And [make him] a messenger to the Children of Israel, [who will say], 'Indeed I have come to you with a sign from your Lord in that I design for you from clay [that which is] like the form of a bird, then I breathe into it and it becomes a bird by permission of Allah. And I cure the blind and the leper, and I give life to the dead - by permission of Allah. And I inform you of what you eat and what you store in your houses. Indeed in that is a sign for you, if you are believers.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi ni wenye kuamini.
Na atamtuma awe Mtume wake kwa Wana wa Israili, (Katika Injili ya Mathayo 15.24 Yesu anasema: Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.- Tazama pia Mathayo 10.5-6 na Mathayo 19.28 na Yohana 17.9) mwenye kutumia hoja za ukweli wa Utume wake kwa miujiza kutokana na Mwenyezi Mungu. Miujiza yenyewe ni kama kufanya kwa udongo sura ya ndege, kisha akipulizia vitaingia uhai na kutaharaki mithili ya ndege kwa atakavyo Mwenyezi Mungu. Pia ataponyesha, kwa kudra ya Mwenyezi Mungu, walio zaliwa vipofu na wataona, na wenye maradhi ya ukoma waondokewe na ukoma, na walio onekana wamekwisha kufa wafufuke. Na yote hayo ni kwa idhini na matakwa ya Mwenyezi Mungu. Pia atawatajia wanacho weka akiba majumbani mwao, vyakula na vyenginevyo. Naye Nabii Isa awaambie: Ishara zote hizi Mwenyezi Mungu amezionyesha kwangu ili iwe hoja kuwa Utume wangu ni wa haki, ikiwa nyinyi ni katika watu wanao tii na kusadiki.(Katika Injili ya Yohana 5.30 Yesu anasema: Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe.)
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Kisha wakarejea kwenye ule ule upotovu wao wakasema: Wewe unajua kwamba hawa hawesemi.
- Basi alipoona mikono yao haimfikilii aliwatilia shaka, na akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Hakika sisi tumetumwa kwa
- Hakika wanao kula mali ya mayatima kwa dhulma, hapana shaka yoyote wanakula matumboni mwao moto,
- Mwenzake akamwambia kwa kubishana naye: Je! Unamkufuru aliye kuumba kutokana na udongo, tena kutokana na
- Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
- Watakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyo pangwa kwa safu. Na tutawaoza mahuru-l-aini.
- Bali hii leo, watasalimu amri.
- Na Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu.
- Wanakuuliza khabarai ya miezi. Sema: Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na
- Atasema Mwenyezi Mungu: Tokomeeni humo, wala msinisemeze.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Al Imran with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Al Imran mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Al Imran Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers