Surah Naml aya 82 , Swahili translation of the meaning Ayah.

  1. Arabic
  2. tafsir
  3. mp3
  4. English
Quran in Swahili QUR,ANI TUKUFU na tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili - Ali Muhsen Alberwany & English - Sahih International : Surah Naml aya 82 in arabic text(The Ants).
  
   

﴿۞ وَإِذَا وَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِمْ أَخْرَجْنَا لَهُمْ دَابَّةً مِّنَ الْأَرْضِ تُكَلِّمُهُمْ أَنَّ النَّاسَ كَانُوا بِآيَاتِنَا لَا يُوقِنُونَ﴾
[ النمل: 82]

Na itapo waangukia kauli juu yao, tutawatolea mnyama katika ardhi atakaye wasemeza, ya kuwa watu walikuwa hawana na yakini na Ishara zetu.

Surah An-Naml in Swahili

Swahili Translation - Al-Barwani

English - Sahih International


And when the word befalls them, We will bring forth for them a creature from the earth speaking to them, [saying] that the people were, of Our verses, not certain [in faith].


Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili


Na itapo waangukia kauli juu yao, tutawatolea mnyama katika ardhi atakaye wasemeza, ya kuwa watu walikuwa hawana na yakini na Ishara zetu.


Na itapo karibia kutimia ahadi ya Mwenyezi Mungu kuileta Saa ya Kiyama na kuwateremshia makafiri adhabu, Mwenyezi Mungu atawatolea watu mnyama kwenye ardhi atakaye waambia miongoni mwa atakayo sema: Hakika makafiri walikuwa hawaiamini miujiza yetu yote, na pia Siku ya Mwisho. Na hayo waliyo kuwa wakiyakanusha sasa yamekwisha kuwa. Na hichi basi kitisho cha hiyo Saa na yanayo fuatia! Hii ndio tafsiri ya Aya hii kwa dhaahiri ya matamko yake. Na zipo tafsiri mbili nyengine ambazo za hii Aya zinazo weza kuwa: Kwanza ni kuwa makusudio ya -Dabbah- ni yeyote aendaye -yadibbu-, katika watu au wengineo. Na hapa inachukuliwa kuwa ni watu, watao kuja kabla ya Kiyama. Na maana yake ni kuwa ikiwateremkia kauli juu yao na adhabu ikathibiti watakuja makundi ya Waumini wakiwaendea, wakienea kote kote, wakizitikisa nguzo za ukafiri. Tafsiri ya pili neno hilo -Dabbah- makusudio yake ni watu waovu, ambao kwa ujinga ni kama wanyama, kama alivyo sema Al Asfahan katika Muqarrarat yake. Na maana yake ni kuwa ikikaribia Siku ya Kiyama, uovu na ufisadi utazidi, na Kiyama wanacho kikanusha makafiri ndio kitakuja. Na hiyo kauli itakuwa, nayo si kauli ya kutamkwa kwa mdomo, lakini kwa kuwa hali yenyewe itakuwa hivyo ni kama iliyo semwa, kama maoni yaliyo kwisha tangulia.

English Türkçe Indonesia
Русский Français فارسی
تفسير Bengali Urdu

listen to Verse 82 from Naml


Ayats from Quran in Swahili


Quran Surah in Swahili :

Al-Baqarah Al-'Imran An-Nisa'
Al-Ma'idah Yusuf Ibrahim
Al-Hijr Al-Kahf Maryam
Al-Hajj Al-Qasas Al-'Ankabut
As-Sajdah Ya Sin Ad-Dukhan
Al-Fath Al-Hujurat Qaf
An-Najm Ar-Rahman Al-Waqi'ah
Al-Hashr Al-Mulk Al-Haqqah
Al-Inshiqaq Al-A'la Al-Ghashiyah

Download Surah Naml with the voice of the most famous Quran reciters :

Surah Naml mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Naml Complete with high quality
Surah Naml Ahmed El Agamy
Ahmed Al Ajmy
Surah Naml Bandar Balila
Bandar Balila
Surah Naml Khalid Al Jalil
Khalid Al Jalil
Surah Naml Saad Al Ghamdi
Saad Al Ghamdi
Surah Naml Saud Al Shuraim
Saud Al Shuraim
Surah Naml Abdul Basit Abdul Samad
Abdul Basit
Surah Naml Abdul Rashid Sufi
Abdul Rashid Sufi
Surah Naml Abdullah Basfar
Abdullah Basfar
Surah Naml Abdullah Awwad Al Juhani
Abdullah Al Juhani
Surah Naml Fares Abbad
Fares Abbad
Surah Naml Maher Al Muaiqly
Maher Al Muaiqly
Surah Naml Muhammad Siddiq Al Minshawi
Al Minshawi
Surah Naml Al Hosary
Al Hosary
Surah Naml Al-afasi
Mishari Al-afasi
Surah Naml Yasser Al Dosari
Yasser Al Dosari


Monday, May 13, 2024

لا تنسنا من دعوة صالحة بظهر الغيب