Surah Nisa aya 92 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ أَن يَقْتُلَ مُؤْمِنًا إِلَّا خَطَأً ۚ وَمَن قَتَلَ مُؤْمِنًا خَطَأً فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ وَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ إِلَّا أَن يَصَّدَّقُوا ۚ فَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ عَدُوٍّ لَّكُمْ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ وَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ فَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ وَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ تَوْبَةً مِّنَ اللَّهِ ۗ وَكَانَ اللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا﴾
[ النساء: 92]
Na haiwi Muumini kumuuwa Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipo kuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni wa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And never is it for a believer to kill a believer except by mistake. And whoever kills a believer by mistake - then the freeing of a believing slave and a compensation payment presented to the deceased's family [is required] unless they give [up their right as] charity. But if the deceased was from a people at war with you and he was a believer - then [only] the freeing of a believing slave; and if he was from a people with whom you have a treaty - then a compensation payment presented to his family and the freeing of a believing slave. And whoever does not find [one or cannot afford to buy one] - then [instead], a fast for two months consecutively, [seeking] acceptance of repentance from Allah. And Allah is ever Knowing and Wise.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na haiwi Muumini kumuuwa Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipo kuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni wa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.
Kuwagawa wanaafiki namna hii ni kwa ajili ya kutoka shakani, ili Muumini asimuuwe Muumini mwenziwe kwa kumdhania kuwa ni mnaafiki. Na haijuzu kumuuwa Muumini ila kwa kukosea, bila ya kukusudia. Na katika hali ya kumuuwa Muumini kwa kukosea akiwa anaishi chini ya utawala wa dola ya Kiislamu, basi atatoa muuwaji diya kuwapa walio fiwa kuwa ni fidia kwa mtu waliye mkosa, na tena amkomboe mtumwa aliye Muumini iwe ni kuwafidia umma wa Kiislamu kwa walicho kosa. Kwani kumkomboa Muumini ni kama kumhuisha mtu kwa kumpatia uhuru. Inakuwa kwa kukomboa shingo ya Muumini ni kuulipa umma wa Kiislamu kwa walicho kosa. Ikiwa aliye uliwa yumo katika watu ambao wana mapatano ya amani na Waislamu, basi yapasa kumpa uhuru mtumwa na kuwalipa watu wa maiti diya, kwani inakuwa hawaichukui hiyo diya kwa kuwaudhi Waislamu kwa sababu ya mapatano yao. Na ikiwa mwenye kuuwa bila ya kukusudia hakupata mtumwa Muumini wa kumkomboa, basi afunge miezi miwili mfululizo, asile mchana hata siku moja. Hayo yawe ni kuitengeza nafsi na kujizoesha kuwa na hadhari zaidi. Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika na Aliye tukuka anazijua sana nafsi za watu na niya zao. Naye ni Mwenye hikima, anajua kuzipanga adhabu zake. -Kuulipa- kwa kuwa utumwa ni amana ya mtu, na kumkomboa mtumwa ni kumhuisha mtu. Akiuliwa Muumini kwa kukosea, na mwenye kuuwa akakomboa shingo ya Muumini basi huyo amehuisha na kuulipa umma.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja.
- Mwenyezi Mungu akasema: Maombi yenu yamekubaliwa. Basi simameni sawa sawa, wala msifuate njia za wale
- Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao.
- Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo.
- Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni
- Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu
- Hao ni wasikilizaji kwa ajili ya kusema uwongo, na ni walaji mno vya haramu! Basi
- Mkiyaepuka makubwa mnayo katazwa, tutakufutieni makosa yenu madogo, na tutakuingizeni mahali patukufu.
- Kisha akaifuata njia.
- Wala msiwape wasio na akili mali yenu ambayo Mwenyezi Mungu ameyajaalia yawe ni kiamu yenu.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers