Surah Anam aya 93 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَيْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَا أَنزَلَ اللَّهُ ۗ وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ﴾
[ الأنعام: 93]
Nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzuliya uwongo Mwenyezi Mungu, au anaye sema: Mimi nimeletewa wahyi; na hali hakuletewa wahyi wowote. Na yule anaye sema: Nitateremsha kama alivyo teremsha Mwenyezi Mungu. Na lau ungeli waona madhaalimu wanavyo kuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyo kuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake.
Surah Al-Anam in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And who is more unjust than one who invents a lie about Allah or says, "It has been inspired to me," while nothing has been inspired to him, and one who says, "I will reveal [something] like what Allah revealed." And if you could but see when the wrongdoers are in the overwhelming pangs of death while the angels extend their hands, [saying], "Discharge your souls! Today you will be awarded the punishment of [extreme] humiliation for what you used to say against Allah other than the truth and [that] you were, toward His verses, being arrogant."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzuliya uwongo Mwenyezi Mungu, au anaye sema: Mimi nimeletewa wahyi; na hali hakuletewa wahyi wowote. Na yule anaye sema: Nitateremsha kama alivyo teremsha Mwenyezi Mungu. Na lau ungeli waona madhaalimu wanavyo kuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyo kuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake.
Nabii huyu hakusema uwongo alipo tangaza kuwa Qurani imetoka kwaMwenyezi Mungu. Na hapana mwenye kumshinda kwa udhaalimu huyo aliye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, au akasema: Nimepata wahyi (ufunuo) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, bila ya kuwa kapata wahyi wowote ule. Vile vile hapana dhaalimu mkubwa zaidi kuliko anaye sema: Mimi nitaleta maneno sawa na hayo aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa unaijua hali ya hao madhaalimu nao wamo katika shida za mauti, na Malaika wanazingoa roho zao kutokana na miili yao, kwa ukali na nguvu, ungeli ona vitisho vya kushitua vinawashukia! Wakati huo hao huambiwa: Sasa malipo yenu ya adhabu ya kudhalilisha na kufedhehesha yanaanza. Malipo haya ni kwa vile mlivyo kuwa mkimzulia Mwenyezi Mungu bila ya haki, na ni malipo kwa kuwa kiburi chenu kilikuzuieni msiangalie na kuzipima Aya, Ishara, za uumbaji za Mwenyezi Mungu ziliomo katika Qurani.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema:
- Wanayo adhabu katika maisha ya dunia, na adhabu ya Akhera hapana shaka ina mashaka zaidi.
- Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.
- Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu.
- Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha.
- Siku hiyo walio kufuru na wakamuasi Mtume watatamani ardhi isawazishwe juu yao. Wala hawataweza kumficha
- Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda
- Naye atakuja ridhika!
- Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata.
- Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anam with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anam mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anam Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers