Surah Maidah aya 95 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْتُلُوا الصَّيْدَ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۚ وَمَن قَتَلَهُ مِنكُم مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاءٌ مِّثْلُ مَا قَتَلَ مِنَ النَّعَمِ يَحْكُمُ بِهِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ هَدْيًا بَالِغَ الْكَعْبَةِ أَوْ كَفَّارَةٌ طَعَامُ مَسَاكِينَ أَوْ عَدْلُ ذَٰلِكَ صِيَامًا لِّيَذُوقَ وَبَالَ أَمْرِهِ ۗ عَفَا اللَّهُ عَمَّا سَلَفَ ۚ وَمَنْ عَادَ فَيَنتَقِمُ اللَّهُ مِنْهُ ۗ وَاللَّهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ﴾
[ المائدة: 95]
Enyi mlio amini! Msiue wanyama wa kuwinda nanyi mmeharimia katika Hija. Na miongoni mwenu atakaye muuwa makusudi, basi malipo yake yatakuwa kwa kuchinja kilicho sawa na alicho kiuwa, katika mifugo, kama wanavyo hukumu waadilifu wawili miongoni mwenu. Mnyama huyo apelekwe kwenye Al Kaaba, au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini; au badala ya hayo ni kufunga, ili aonje ubaya wa jambo lake hili. Mwenyezi Mungu amekwisha yafuta yaliyo pita; lakini atakaye fanya tena Mwenyezi Mungu atampa adhabu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu na Mwenye kuadhibu.
Surah Al-Maidah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
O you who have believed, do not kill game while you are in the state of ihram. And whoever of you kills it intentionally - the penalty is an equivalent from sacrificial animals to what he killed, as judged by two just men among you as an offering [to Allah] delivered to the Ka'bah, or an expiation: the feeding of needy people or the equivalent of that in fasting, that he may taste the consequence of his deed. Allah has pardoned what is past; but whoever returns [to violation], then Allah will take retribution from him. And Allah is Exalted in Might and Owner of Retribution.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Enyi mlio amini! Msiue wanyama wa kuwinda nanyi mmeharimia katika Hija. Na miongoni mwenu atakaye muuwa makusudi, basi malipo yake yatakuwa kwa kuchinja kilicho sawa na alicho kiuwa, katika mifugo, kama wanavyo hukumu waadilifu wawili miongoni mwenu. Mnyama huyo apelekwe kwenye Al Kaaba, au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini; au badala ya hayo ni kufunga, ili aonje ubaya wa jambo lake hili. Mwenyezi Mungu amekwisha yafuta yaliyo pita; lakini atakaye fanya tena Mwenyezi Mungu atampa adhabu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu na Mwenye kuadhibu.
Enyi ambao mmeamini! Msiuwe nyama wa kuwinda nanyi mmenuia Hija na Umra na mmo kuzitimiliza. Na mwenye kumuuwa mnyama kama huyo kwa kukusudia basi itampasa atoe fidiya mfano wa mnyama aliye muuwa, ikiwa katika ngamia, ngombe au kondoo. Na hujuulikana huyo mfano wake kwa kukadiriwa na watu wawili waadilifu kati yenu, wahukumu na wawape mafakiri kwenye Al Kaaba, au atoe badala yake awape, au atoe chakula kadiri ya yule mnyama kuwapa mafakiri. Kila fakiri apewe chakula cha kumtosha kutwa yake. Hayo ndio kuondoa dhambi za kuwinda kuliko katazwa. Au badala ya hayo yote, afunge idadi ya siku za kadri ya wale masikini iliyo mbidi kuwalisha lau angewalisha. Na Mwenyezi Mungu amelazimisha hayo ili huyo mwenye kufanya lile kosa apate kuhisi matokeo ya kosa lake na uwovu wa malipo yake. Mwenyezi Mungu, lakini, amesamehe ukhalifu ulio tendekea kabla ya jambo hilo halijaharimishwa. Na mwenye kurejea tena kufanya uovu baada ya kujua kuwa ni haramu, basi hakika Mwenyezi Mungu atampa adabu kwa kitendo chake, naye Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushinda hashindiki, Mkali wa kumuadhibu anaye kakamia kutenda dhambi. (Tunaona kuwa Uislamu ulianzisha kulinda mazingara, na utajiri wa asili tangu hapo kale. Kutokana na kuhifadhiwa wanyama na ndege wa porini huko Makka, ndio hii leo tunaona zipo nyanda na mapori yanayo hifadhiwa wanyama wake, kwa mujibu wa utaalamu wa kisasa.)
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni.
- Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya
- Naye ndiye anaye pokea toba kwa waja wake, na anasamehe makosa, na anayajua mnayo yatenda.
- Na miji mingapi iliyo jifakharisha tumeiangamiza! Na hayo maskani yao hayakukaliwa tena baada yao, ila
- Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima.
- Basi subiri kwa subira njema.
- Wakizikataa neema tulizo wapa. Basi stareheni. Mtakuja jua!
- Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu?
- Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu ende kwa Firauni na waheshimiwa wake,
- Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers