Surah Araf aya 95 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿ثُمَّ بَدَّلْنَا مَكَانَ السَّيِّئَةِ الْحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَوا وَّقَالُوا قَدْ مَسَّ آبَاءَنَا الضَّرَّاءُ وَالسَّرَّاءُ فَأَخَذْنَاهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ﴾
[ الأعراف: 95]
Kisha Sisi hubadilisha mahala pa ubaya kwa wema, hata wakazidi, na wakasema: Taabu na raha ziliwafikia baba zetu. Basi kwa ghafla tukawashika, hali ya kuwa hawajatambua.
Surah Al-Araf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Then We exchanged in place of the bad [condition], good, until they increased [and prospered] and said, "Our fathers [also] were touched with hardship and ease." So We seized them suddenly while they did not perceive.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Kisha Sisi hubadilisha mahala pa ubaya kwa wema, hata wakazidi, na wakasema: Taabu na raha ziliwafikia baba zetu. Basi kwa ghafla tukawashika, hali ya kuwa hawajatambua.
Basi tena ilivyo kuwa hawakufanya hayo, bali wakaendelea na ukafiri wao na inadi yao, tukawapa mtihani wa kuwapa neema badala ya dhiki ili kuwapururia tu. Tukawapa kutononoka, na nafasi nzuri, na siha na afya, mpaka wakawa wengi, na mali yao yakazidi, wakasema kwa ujinga wao: Hayo yaliyo wapata baba zetu ya mahna, na balaa, na starehe na neema - hayo yote ndio shani ya ulimwengu. Shida na neema huwajia watu kwa zamu. Hawakuzindukana wakajua kuwa haya ni malipo ya kufru zao wakajizuia! Na kwa hivyo wakawa hawaujui mwendo wa Mwenyezi Mungu, iliyo tukuka shani yake, katika sababu za matengenezo na uharibifu wa binaadamu, na nini linalo leta neema na nini linalo leta dhiki! Matokeo ya hayo ni kuwa Mwenyezi Mungu aliwapatiliza kwa kuwaletea adhabu ya kuteketeza kwa ghafla, na wao bila ya kujua nini litawafika.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na akitoroka yeyote katika wake zenu kwenda kwa makafiri, tena ikatokea mkapata ngawira, basi wapeni
- Mwenye kutua, akatulia,
- Aliye umba mbingu saba kwa matabaka. Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema.
- Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake;
- Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye amemteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kina upogo.
- Kisha akatazama,
- Naye ndiye aliye fanya usiku na mchana kufuatana kwa nafuu ya anaye taka kukumbuka, au
- (Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo.
- Basi mnakwenda wapi?
- Ambao waliziamini Ishara zangu na walikuwa Waislamu.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Araf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Araf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Araf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers