La sourate Abasa en Swahili
عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ(1) Alikunja kipaji na akageuka, |
أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ(2) Kwa sababu alimjia kipofu! |
وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ(3) Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika? |
أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ(4) Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? |
أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ(5) Ama ajionaye hana haja, |
فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ(6) Wewe ndio unamshughulikia? |
وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ(7) Na si juu yako kama hakutakasika. |
وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ(8) Ama anaye kujia kwa juhudi, |
وَهُوَ يَخْشَىٰ(9) Naye anaogopa, |
فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ(10) Ndio wewe unampuuza? |
كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ(11) Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana. |
فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ(12) Basi anaye penda akumbuke. |
فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ(13) Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa, |
مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ(14) Zilizo inuliwa, zilizo takaswa. |
بِأَيْدِي سَفَرَةٍ(15) Zimo mikononi mwa Malaika waandishi, |
كِرَامٍ بَرَرَةٍ(16) Watukufu, wema. |
قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ(17) Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha? |
مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ(18) Kwa kitu gani amemuumba? |
مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ(19) Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria. |
ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ(20) Kisha akamsahilishia njia. |
ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ(21) Kisha akamfisha, akamtia kaburini. |
ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنشَرَهُ(22) Kisha apendapo atamfufua. |
كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ(23) La! Hajamaliza aliyo muamuru. |
فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ(24) Hebu mtu na atazame chakula chake. |
أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا(25) Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu, |
ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا(26) Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu, |
فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا(27) Kisha tukaotesha humo nafaka, |
وَعِنَبًا وَقَضْبًا(28) Na zabibu, na mimea ya majani, |
وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا(29) Na mizaituni, na mitende, |
وَحَدَائِقَ غُلْبًا(30) Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara, |
وَفَاكِهَةً وَأَبًّا(31) Na matunda, na malisho ya wanyama; |
مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ(32) Kwa manufaa yenu na mifugo yenu. |
فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ(33) Basi utakapo kuja ukelele, |
يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ(34) Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, |
وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ(35) Na mamaye na babaye, |
وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ(36) Na mkewe na wanawe - |
لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ(37) Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha. |
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ(38) Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri, |
ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ(39) Zitacheka, zitachangamka; |
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ(40) Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi, |
تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ(41) Giza totoro litazifunika, |
أُولَٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ(42) Hao ndio makafiri watenda maovu. |
Plus de sourates en Swahili :
Téléchargez la sourate avec la voix des récitants du Coran les plus célèbres :
Téléchargez le fichier mp3 de la sourate Abasa : choisissez le récitateur pour écouter et télécharger la sourate Abasa complète en haute qualité.















Donnez-nous une invitation valide