La sourate Al-Balad en Swahili
لَا أُقْسِمُ بِهَٰذَا الْبَلَدِ(1) Naapa kwa Mji huu! |
وَأَنتَ حِلٌّ بِهَٰذَا الْبَلَدِ(2) Nawe unaukaa Mji huu. |
وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ(3) Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. |
لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي كَبَدٍ(4) Hakika tumemuumba mtu katika taabu. |
أَيَحْسَبُ أَن لَّن يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌ(5) Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? |
يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًا لُّبَدًا(6) Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. |
أَيَحْسَبُ أَن لَّمْ يَرَهُ أَحَدٌ(7) Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? |
أَلَمْ نَجْعَل لَّهُ عَيْنَيْنِ(8) Kwani hatukumpa macho mawili? |
وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ(9) Na ulimi, na midomo miwili? |
وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ(10) Na tukambainishia zote njia mbili? |
فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ(11) Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. |
وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ(12) Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? |
فَكُّ رَقَبَةٍ(13) Kumkomboa mtumwa; |
أَوْ إِطْعَامٌ فِي يَوْمٍ ذِي مَسْغَبَةٍ(14) Au kumlisha siku ya njaa |
يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ(15) Yatima aliye jamaa, |
أَوْ مِسْكِينًا ذَا مَتْرَبَةٍ(16) Au masikini aliye vumbini. |
ثُمَّ كَانَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا بِالْمَرْحَمَةِ(17) Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. |
أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ(18) Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. |
وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا هُمْ أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ(19) Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. |
عَلَيْهِمْ نَارٌ مُّؤْصَدَةٌ(20) Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande. |
Plus de sourates en Swahili :
Téléchargez la sourate avec la voix des récitants du Coran les plus célèbres :
Téléchargez le fichier mp3 de la sourate Al-Balad : choisissez le récitateur pour écouter et télécharger la sourate Al-Balad complète en haute qualité.















Donnez-nous une invitation valide