Surah Raad aya 1 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿المر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ ۗ وَالَّذِي أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ الْحَقُّ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ﴾
[ الرعد: 1]
Alif Lam Mym Ra. (A. L. M. R.) Hizi ni Ishara za Kitabu. Na uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki. Lakini wengi wa watu hawaamini.
Surah Ar-Rad in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Alif, Lam, Meem, Ra. These are the verses of the Book; and what has been revealed to you from your Lord is the truth, but most of the people do not believe.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Alif Lam Mym Ra. (A.L.M.R.) Hizi ni Ishara za Kitabu. Na uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki. Lakini wengi wa watu hawaamini.
-Alif Mym Ra- hizi ni harufi za kutamkwa zimeanzia baadhi ya Sura za Qurani. Nazo zinaashiria kuwa huu ni muujiza juu ya kuwa ni harufi wanazo zitumia Waarabu katika maneno yao ya kawaida! Na harufi hizi zilikuwa zikitamkwa huwavutia Waarabu waisikilize Qurani! Kwani wale mapagani (washirikina) waliambizana wasiisikilize hii Qurani. Ikawa Waumini wakianzia harufi hizi huvutia masikio ya washirikina wakawa wanasikiliza. Hakika hizo Aya au Ishara tukufu ndio hii Qurani, Kitabu chenye shani kubwa, uliyo teremshiwa wewe Nabii kwa haki na ukweli kutokana na Mwenyezi Mungu, aliye kuumba, na akakuteuwa. Lakini wengi wa washirikina walio yakanya yaliyo kuja ya Haki si watu wa kuikubali Haki. Bali wao wanaipinga kwa inda.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Ewe baba yangu! Kwa yakini imenifikia ilimu isiyo kufikia wewe. Basi nifuate mimi, nami nitakuongoza
- Kisha hakika Mola wako Mlezi kwa walio tenda uovu kwa ujinga, kisha wakatubia baada ya
- Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema:
- Na wanapo ambiwa: Kateremsha nini Mola wenu Mlezi? Husema: Hadithi za kubuni za watu wa
- Hakika wale wanao upotoa ukweli uliomo katika Ishara zetu hawatufichikii Sisi. Je! Atakaye tupwa Motoni
- Musa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua.
- Na siku watakapo letwa walio kufuru kwenye Moto wataambiwa: Nyinyi mlitwaa vitu vyenu vizuri katika
- Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi.
- Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda
- Na badala ya Mwenyezi Mungu wanawaabudu wasio wamilikia riziki kutoka mbinguni wala kwenye ardhi, wala
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Raad with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Raad mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Raad Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



