Surah Nisa aya 119 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّهِ ۚ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا﴾
[ النساء: 119]
Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo umba Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya Shet'ani kuwa ni mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu, basi huyo amekhasiri khasara ya dhaahiri.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And I will mislead them, and I will arouse in them [sinful] desires, and I will command them so they will slit the ears of cattle, and I will command them so they will change the creation of Allah." And whoever takes Satan as an ally instead of Allah has certainly sustained a clear loss.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo umba Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya Shetani kuwa ni mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu, basi huyo amekhasiri khasara ya dhaahiri.
Hakika kiapo chake Shetani ni kuwa atawapoteza wale anao wapumbaza kwa kuwatenga mbali na Haki, na kuchochea pumbao lao na matamanio yao, mpaka wakawa wamepotea wanatanga tanga katika mawazo na tamaa za uwongo. Wakisha kuwa katika kuzainiwa huku na tamaa hizo chini ya utawala wake Shetani, tena huwatokomeza kwenye mambo yasiyo ingia akilini, na huwapelekea hao wafikiri kufanya hayo ni ibada. Na ilhali haya yote ni mawazo ya uwongo tu. Basi huwatia wasiwasi wakatenda mambo, kama kwa mfano kuwakata masikio baadhi ya ngamia wao, wageuze khulka aliyo iumba Mwenyezi Mungu. Wakafanya kuwa ngamia aliye katwa masikio yake hachinjwi, wala hafanyishwi kazi, wala hazuiliwi kwenda machungani atakavyo. Yote haya ni kwa amri yake Shetani kuwazaini. Tena huwatia wasiwasi mpaka wakaona kuwa hayo ni katika dini. Na hakika wao inakuwa wanamfuata yeye Shetani, na wanamfanya yeye ndiye wa kuwanusuru, na ndiye wa kumfuata badala ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya Shetani ndiye msaidizi wake wa kumfuata, basi amekhasiri khasara kubwa iliyo wazi. Kwani hapo anakuwa amepotea njia ya Haki, na ameipumbaza akili yake, na utampata ufisadi duniani, na adhabu Akhera.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na walipo sema wanaafiki, na wale wenye ugonjwa nyoyoni mwao: Watu hawa dini yao imewadanganya.
- Wala hamhimizani kulisha masikini;
- Hakika vinyama vilio viovu kabisa mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale wanao kufuru, basi hao
- Na Ismail, na Idris, na Dhulkifli - wote walikuwa miongoni mwa wanao subiri.
- Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi.
- Na kama amempa t'alaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe
- Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala
- Na Mwenyezi Mungu aliwarudisha nyuma makafiri juu ya ghadhabu yao; hawakupata kheri yoyote. Na Mwenyezi
- Ametukuka aliye teremsha Furqani kwa mja wake, ili awe mwonyaji kwa walimwengu wote.
- Hakika haya ndiyo maelezo ya kweli. Na hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu tu, na hakika
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers