Surah Nisa aya 142 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوا إِلَى الصَّلَاةِ قَامُوا كُسَالَىٰ يُرَاءُونَ النَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ اللَّهَ إِلَّا قَلِيلًا﴾
[ النساء: 142]
Hakika wanaafiki wanamkhadaa Mwenyezi Mungu, na hali ni Yeye ndiye mwenye kuwakhadaa wao. Na wanapo inuka kusali huinuka kwa unyong'onyo, wanajionyesha kwa watu tu, wala hawamdhukuru Mwenyezi Mungu ila kidogo tu.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Indeed, the hypocrites [think to] deceive Allah, but He is deceiving them. And when they stand for prayer, they stand lazily, showing [themselves to] the people and not remembering Allah except a little,
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Hakika wanaafiki wanamkhadaa Mwenyezi Mungu, na hali ni Yeye ndiye mwenye kuwakhadaa wao. Na wanapo inuka kuswali huinuka kwa unyongonyo, wanajionyesha kwa watu tu, wala hawamdhukuru Mwenyezi Mungu ila kidogo tu.
Hakika wanaafiki, kwa ule unaafiki wao, wanadhani kuwa wanamkhadaa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wanamficha hakika ya nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Yeye ndiye anaye wakhadaa wao. Basi Yeye huwapururia kuwapa muhula, na anawawacha mpaka wabobee katika maovu yao, kisha ndio awahisabu kwa waliyo yatenda. Na hawa wanaafiki wana dhaahiri ya kuonekana, na ya ndani ya nafsi zao. Yale ya kuonekana ni vile kuwa wakiinuka kwenda kuswali huinuka kwa uvivu, kwa unyongonyo. Na Swala yao ni riya tu, kuonyesha, si ya kweli. Na ya ndani ni kuwa hawakumbuki kumtaja Mwenyezi Mungu ila kwa nadra, kwa tukizi. Na lau kuwa wanamkumbuka vilivyo wangeli uacha unaafiki
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na Shet'ani amewapambia vitendo
- Na wanampa Mwenyezi Mungu wanavyo vichukia wao, na ndimi zao zinasema uwongo kwamba wao watapata
- Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha.
- Je! Anaye kwenda akisinukia juu ya uso wake ni mwongofu zaidi, au yule anaye kwenda
- Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika checmchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu.
- Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi tukufu..
- Wakamkanusha. Basi tukamwokoa, pamoja na walio kuwa naye, katika jahazi. Na tukawafanya wao ndio walio
- Hakika hao wanao bishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu bila ya uthibitisho wowote uliyo wajia,
- Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni. Kisha akayapitisha kwenye chemchem katika ardhi,
- Kwa anaye taka miongoni mwenu kutangulia au kuchelewa.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers