Surah Nisa aya 141 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿الَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمْ فَإِن كَانَ لَكُمْ فَتْحٌ مِّنَ اللَّهِ قَالُوا أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ وَإِن كَانَ لِلْكَافِرِينَ نَصِيبٌ قَالُوا أَلَمْ نَسْتَحْوِذْ عَلَيْكُمْ وَنَمْنَعْكُم مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ ۚ فَاللَّهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَلَن يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا﴾
[ النساء: 141]
Wale ambao wanakungojeeni, mkipata ushindi unao toka kwa Mwenyezi Mungu wao husema: Si tulikuwa pamoja nanyi vile? Na ikiwa ni sehemu ya makafiri kushinda wao huwaambia: Hatukuwa ni waweza wa kukushindeni, nasi tukakukingeni na hawa Waumini? Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama, wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Those who wait [and watch] you. Then if you gain a victory from Allah, they say, "Were we not with you?" But if the disbelievers have a success, they say [to them], "Did we not gain the advantage over you, but we protected you from the believers?" Allah will judge between [all of] you on the Day of Resurrection, and never will Allah give the disbelievers over the believers a way [to overcome them].
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Wale ambao wanakungojeeni, mkipata ushindi unao toka kwa Mwenyezi Mungu wao husema: Si tulikuwa pamoja nanyi vile? Na ikiwa ni sehemu ya makafiri kushinda wao huwaambia: Hatukuwa ni waweza wa kukushindeni, nasi tukakukingeni na hawa Waumini? Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama, wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.
Mtindo wa wanaafiki ni kukungojeeni kama anavyo ngojea mwenye husda na maya anaye tamani mpate masaibu mnapo kuwa katika vita na maadui. Mkishinda kwa nusra ya Mwenyezi Mungu, na mkafungukiwa njia ya Haki, wao huwaambia Waumini - na hali wao ule ushindi walio pewa wenye Imani na Mwenyezi Mungu umewashtusha : Sisi hatukuwa nanyi? Kwa maana sisi ni jamaa zenu! Na ikiwa ni zamu ya makafiri kupata ushindi, basi wao huwaendea na kuwaambia: Sisi hatukuyashughulikia mambo yenu hata yakawa ni yetu? Na hatukukupeni mapenzi yetu, na tukakulindeni na hawa Waumini? (yaani sisi ni wenzenu). Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala atakuhukumuni baina yenu na hawa wanaafiki Siku ya Kiyama. Wala Mwenyezi Mungu hatowapa makafiri njia kuwashinda Waumini maadamu Waumini watashikamana na sifa ya Imani ya kweli na vitendo vyema.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na mkifa au mkiuliwa ni kwa Mwenyezi Mungu ndio mtakusanywa.
- Pindi wakitolewa hawatatoka pamoja nao, na wakipigwa vita hawatawasaidia. Na kama wakiwasaidia basi watageuza migongo;
- Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo,
- Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko?
- Sema: Nyinyi mnayo miadi ya Siku ambayo hamtaakhirika nayo kwa saa moja, wala hamtaitangulia.
- Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni.
- Na ukiwauliza, wanasema: Sisi tulikuwa tukipiga porojo na kucheza tu. Sema: Mlikuwa mkimfanyia maskhara Mwenyezi
- Na wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa
- Na Mwenyezi Mungu aliwarudisha nyuma makafiri juu ya ghadhabu yao; hawakupata kheri yoyote. Na Mwenyezi
- Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers