Surah Araf aya 158 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴾
[ الأعراف: 158]
Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliye tumwa na Mwenyezi Mungu Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mungu ila Yeye anaye huisha na anaye fisha. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake asiyejua kusoma na kuandika, ambaye anamuamini Mwenyezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka.
Surah Al-Araf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Say, [O Muhammad], "O mankind, indeed I am the Messenger of Allah to you all, [from Him] to whom belongs the dominion of the heavens and the earth. There is no deity except Him; He gives life and causes death." So believe in Allah and His Messenger, the unlettered prophet, who believes in Allah and His words, and follow him that you may be guided.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliye tumwa na Mwenyezi Mungu Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mungu ila Yeye anaye huisha na anaye fisha. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake asiyejua kusoma na kuandika, ambaye anamuamini Mwenyezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka.
Ewe Nabii! Waambie watu: Hakika mimi nimetumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi nyote, bila ya farka baina ya Mwaarabu na asiye kuwa Mwaarabu, baina ya mweusi na mweupe. Na Mwenyezi Mungu aliye nituma ni Yeye peke yake ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Huipitisha amri yake kwa mujibu wa hikima yake. Na hufanya mbinguni na duniani kama anavyo penda. Wala hapana wa kuabudiwa kwa haki ila Yeye. Na Yeye ndiye Mwenye uwezo wa kuhuisha na kufisha, wala hapana mwenginewe. Basi muaminini Yeye na Mtume wake, huyu Nabii asiye soma wala kuandika. Naye huyu anamuamini Mwenyezi Mungu ambaye anaye kuiteni mumuamini. Na anaamini Vitabu vyake vilivyo teremshwa. Basi mfuateni katika kila afanyalo na asemalo mpate kuongoka na kuongozeka.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Au hawakumjua Mtume wao, ndio maana wanamkataa?
- Wala msiwaoe wake walio waoa baba zenu, ila yaliyo kwisha pita. Hakika huo ni uchafu
- Je! Imekufikia hadithi ya Musa?
- Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.
- Au hatawashika kwa kitisho na kuwapunguza kidogo kidogo? Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye huruma,
- Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa mbingu
- Enyi mlio amini! Yanapo mfikia mauti mmoja wenu na akataka kutoa wasia, basi wawepo mashahidi
- Kisha baada yake tukawatuma Mitume kwa watu wao. Nao wakawajia kwa Ishara zilizo wazi. Lakini
- Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka?
- Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata kinacho
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Araf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Araf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Araf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers