Surah Ahzab aya 19 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَشِحَّةً عَلَيْكُمْ ۖ فَإِذَا جَاءَ الْخَوْفُ رَأَيْتَهُمْ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ تَدُورُ أَعْيُنُهُمْ كَالَّذِي يُغْشَىٰ عَلَيْهِ مِنَ الْمَوْتِ ۖ فَإِذَا ذَهَبَ الْخَوْفُ سَلَقُوكُم بِأَلْسِنَةٍ حِدَادٍ أَشِحَّةً عَلَى الْخَيْرِ ۚ أُولَٰئِكَ لَمْ يُؤْمِنُوا فَأَحْبَطَ اللَّهُ أَعْمَالَهُمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرًا﴾
[ الأحزاب: 19]
Wana choyo juu yenu. Ikifika khofu utawaona wanakutazama na macho yao yanazunguka, kama yule ambaye aliye zimia kwa kukaribia mauti. Na khofu ikiondoka wanakuudhini kwa ndimi kali, nao ni mabakhili kwa kila la kheri. Hao hawakuamini, basi Mwenyezi Mungu amevibat'ilisha vitendo vyao. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.
Surah Al-Ahzab in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Indisposed toward you. And when fear comes, you see them looking at you, their eyes revolving like one being overcome by death. But when fear departs, they lash you with sharp tongues, indisposed toward [any] good. Those have not believed, so Allah has rendered their deeds worthless, and ever is that, for Allah, easy.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Wana choyo juu yenu. Ikifika khofu utawaona wanakutazama na macho yao yanazunguka, kama yule ambaye aliye zimia kwa kukaribia mauti. Na khofu ikiondoka wanakuudhini kwa ndimi kali, nao ni mabakhili kwa kila la kheri. Hao hawakuamini, basi Mwenyezi Mungu amevibatilisha vitendo vyao. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.
Wana pupa juu yenu kwa kuonekana dhaahiri inapo kuwa hapana khofu. Na ikija khofu ya adui au ya Mtume s.a.w. utawaona wanakuangalia na macho yao yanawazunguka hawajitambui, kama hali ya mwenye kuzimia wakati wa sumbuko la kukaribia mauti. Na khofu ikiondoka wanapita mpaka kukutukaneni na kukushutumuni kwa ndimi za kukata. Hao ni mabakhili kwa kila la kheri. Hao hawakuamini kwa nyoyo zao, ijapo kuwa wametangaza kuwa ni Waislamu. Basi Mwenyezi Mungu amezibatilisha amali zao kwa ukafiri wao walio dhamiria. Na kubatilisha huko ni jambo jepesi kwa Mwenyezi Mungu. Aya hii tukufu inaashiria ukweli wa kisayansi ambao ulikuwa haukujuulikana namna yake wakati wa kuteremka Qurani Tukufu. Ukweli huo ni kuwa jicho wakati wa kukurubia mauti au wakati wa khofu huzunguka. Na katika sababu za hayo ni kuwa kwa shida ya khofu utambuzi hutoweka, ikawa mtu hajitambui. Vituo vya navo zisio tambua katika ubongo hupoteza mizani yake, basi huwa huyo mwenye khofu kama mfano wa mwenye kuzimia kwa kukaribia kufa, jicho lake huzunguka na mboni ya jicho hupanuka, na hubaki katika hali ya kukodoa macho mpaka kufa.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Au maji yake yakadidimia wala usiweze kuyagundua.
- Zilizo tiwa alama kwa Mola wako Mlezi. Na haya hayako mbali na wenye kudhulumu wengineo.
- Siku hiyo nyoyo zitapiga piga,
- Na Sisi ndio tunao huisha na tunao fisha. Na Sisi ndio Warithi.
- Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akateremsha maji kutoka mbinguni. Na kwa
- Na lau kuwa Mwenyezi Mungu asingeli waandikia kutoka, angeli waadhibu katika dunia. Na katika Akhera
- Na watakapo tupwa humo mahali dhiki, hali wamefungwa, wataomba wafe.
- Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu.
- Hakika tuliwajaribu walio kuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli
- Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Ahzab with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Ahzab mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Ahzab Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers