Surah Mulk aya 5 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَلَقَدْ زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَجَعَلْنَاهَا رُجُومًا لِّلشَّيَاطِينِ ۖ وَأَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابَ السَّعِيرِ﴾
[ الملك: 5]
Na kwa hakika tumeipamba mbingu ya karibu kwa mataa, na tumeyafanya ili kuwapigia mashetani, na tumewaandalia adhabu ya Moto uwakao kwa nguvu.
Surah Al-Mulk in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And We have certainly beautified the nearest heaven with stars and have made [from] them what is thrown at the devils and have prepared for them the punishment of the Blaze.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na kwa hakika tumeipamba mbingu ya karibu kwa mataa, na tumeyafanya ili kuwapigia mashetani, na tumewaandalia adhabu ya Moto uwakao kwa nguvu.
Na hakika Sisi tumeipamba mbingu hii ya karibu, unayo iona kwa macho, tumeipamba kwa nyota zinazo ngaa. Na tumefanya katika hizo vimondo vya kuwapopolea mashetani; na Akhera tumewaandalia adhabu ya moto unao waka. Mbingu ni kila kilicho juu yetu kikatufunika. Amesema Ibn Sayyidih: Hiyo ni bahari ya anga na vyombo vyote viliomo ndani yake na vimondo. Na sura wanayo iona wakaazi wa duniani katika masiku yaliyo safi ni kama qubba la kibuluu lilio pambwa kwa nyota na sayari kama kwamba ni taa, kama unavyo ziona nyota za mkia, au vimondo, vinakwenda angani vikiungua huko juu ya ardhi. Na hilo qubba la kibuluu si chochote ila ni matokeo ya mwangaza wa jua na nyota pamoja na takataka za vumbi zinazo ninginia katika hewa, na sehemu za hewa molecules zinazo tawanyika. Haya mbali na yanayo onekana katika mwangaza nafsi yake ambayo huipamba mbingu hii ya karibu, kama vile zile rangi nzuri nzuri za wakati wa kuchwa jua, au wakati wa kuchomoza jua alfajiri, na mianga ya njia za nyota, miangaza ya kaskazini, na miangaza ya katika sehema za Polar regions. Na hayo yote yanayo onekana ni matokeo ya kuingiliana mwanga pamoja na funiko la anga la ardhi na uwanja wake wa smaku, magnetic field.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Sisi tunasimulia simulizi nzuri kwa kukufunulia Qur'ani hii. Na ijapo kuwa kabla ya haya ulikuwa
- Sema: Lau kuwa ninacho hicho mnacho kihimiza, ingeli kwisha katwa shauri baina yangu na nyinyi.
- Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
- Hamkuwauwa nyinyi lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye wauwa. Na wewe hukutupa, walakini Mwenyezi Mungu ndiye
- Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na
- Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana.
- Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote
- Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Mulk with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Mulk mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Mulk Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers