Surah Fatir aya 41 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ إِنَّ اللَّهَ يُمْسِكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ أَن تَزُولَا ۚ وَلَئِن زَالَتَا إِنْ أَمْسَكَهُمَا مِنْ أَحَدٍ مِّن بَعْدِهِ ۚ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا﴾
[ فاطر: 41]
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anaye zuilia mbingu na ardhi zisiondoke. Na zikiondoka hapana yeyote wa kuzizuia isipo kuwa Yeye. Hakika Yeye ni Mpole Mwenye kusamehe.
Surah Fatir in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Indeed, Allah holds the heavens and the earth, lest they cease. And if they should cease, no one could hold them [in place] after Him. Indeed, He is Forbearing and Forgiving.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anaye zuilia mbingu na ardhi zisiondoke. Na zikiondoka hapana yeyote wa kuzizuia isipo kuwa Yeye. Hakika Yeye ni Mpole Mwenye kusamehe.
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anaye zuia mpango wa mbingu na ardhi usivurugike, na ndiye anaye zihifadhi mbingu na ardhi zisiondoke. Na lau akizijaalia kuondoka hapana wa kuweza kuzihifadhi hizo isipo kuwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe. Hakika Yeye ni Mpole, hafanyi papara kuwaadhibu wakhalifu. Yeye ni Msamehevu wa madhambi ya wenye kurejea kwake wakatubu. Aya hii tukufu inathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala peke yake ndiye Muumba mbingu na ardhi. Yeye ndiye Mwenye kuzishika zisiondoke. Kwani hivi vitu viliomo mbinguni vya karibu na mbali vinavyo onekana katika qubba la mbingu vimeshikamana kwa mujibu wa mpango maalumu wa namna ya pekee alio uumba Mwenyezi Mungu Aliye takasika na Kutukuka. Na Yeye ndiye aliye viwekea mvutano usio katika kwa kupita zama na vizazi, na ndiye anaye vihifadhi visikosee mizani yao. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala ndiye Mwenye uweza huu, wala hapana mwenginewe.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Akasema: Ewe Nuhu! Huyu si katika ahali zako. Mwendo wake si mwema. Basi usiniombe jambo
- Akasema: Hakika humo yumo Lut'i. Wao wakasema: Sisi tunajua zaidi nani yumo humo. Hapana shaka
- Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu!
- Ya Firauni na Thamudi?
- Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.
- Hakika Sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali.
- Humuomba yule ambaye bila ya shaka dhara yake ipo karibu zaidi kuliko nafuu yake. Kwa
- Na tukamsahilishia Suleiman upepo wa kimbunga wendao kwa amri yake kwenye ardhi tuliyo ibarikia. Na
- Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anaye taka
- Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Fatir with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Fatir mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Fatir Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers