Surah Yunus aya 22 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿هُوَ الَّذِي يُسَيِّرُكُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا كُنتُمْ فِي الْفُلْكِ وَجَرَيْنَ بِهِم بِرِيحٍ طَيِّبَةٍ وَفَرِحُوا بِهَا جَاءَتْهَا رِيحٌ عَاصِفٌ وَجَاءَهُمُ الْمَوْجُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ أُحِيطَ بِهِمْ ۙ دَعَوُا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ لَئِنْ أَنجَيْتَنَا مِنْ هَٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ﴾
[ يونس: 22]
Yeye ndiye anaye kuendesheni bara na baharini. Hata mnapo kuwa majahazini na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakaufurahia, upepo mkali ukawazukia, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakaona wamesha zongwa, basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia niya: Ukituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru.
Surah Yunus in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
It is He who enables you to travel on land and sea until, when you are in ships and they sail with them by a good wind and they rejoice therein, there comes a storm wind and the waves come upon them from everywhere and they assume that they are surrounded, supplicating Allah, sincere to Him in religion, "If You should save us from this, we will surely be among the thankful."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Yeye ndiye anaye kuendesheni bara na baharini. Hata mnapo kuwa majahazini na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakaufurahia, upepo mkali ukawazukia, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakaona wameshazongwa, basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia niya: Ukituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru.
Mwenyezi Mungu mnaye ikufuru neema yake, na mnakanusha Ishara zake, ndiye Yeye anaye kuezesheni kwenda na kutembea nchi kavu kwa miguu au kwa vipando, na baharini kwa vyombo alivyo fanya vikutumikieni, vinavyo kwenda juu ya maji, kama anavyo visahilishia Mwenyezi Mungu kwa upepo mzuri unao puliza kwa amani mpaka kufikilia huko vyendako. Hata mkisha tumaini na mkafurahia huvuma tena upepo mkali ukatibua mawimbi kutoka kila upande, na mkayakinika kuwa hapana ila kuhiliki tu! Katika shida kama hii hamna tegemeo ila Mwenyezi Mungu. Hapo basi mnamwomba madua kwa usafi wa niya, kwa kuyakinika kuwa hapana mwokozi isipo kuwa Yeye, na mnampa ahadi kuwa pindi akikuvueni na balaa hiyo mtamuamini, na mtakuwa wenye kushukuru.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hamuabudu badala yake ila majina tu mliyo yapanga nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia
- Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Sala,
- Na lau kuwa hatukukuweka imara ungeli karibia kuwaelekea kidogo.
- Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
- Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu
- Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa wote.
- Ukikupata wema unawachukiza, na ukikusibu msiba, wao husema: Sisi tuliangalia mambo yetu vizuri tangu kwanza.
- Hizi ni katika khabari za ghaibu tunazo kufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala watu wako, kabla
- Sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Muumba mbingu na ardhi! Mjuzi wa yasiyo onekana na yanayo onekana!
- Na alipanda kiburi yeye na majeshi yake katika nchi bila ya haki, na wakadhania kuwa
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yunus with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yunus mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yunus Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers