Surah Nasr aya 3 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُ ۚ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا﴾
[ النصر: 3]
Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba.
Surah An-Nasr in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Then exalt [Him] with praise of your Lord and ask forgiveness of Him. Indeed, He is ever Accepting of repentance.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba.
Basi mshukuru Mola wako Mlezi, na Sabbih , Mtakase kwa sifa zake, na mtake akusamehe wewe na umma wako, kwani hakika Yeye ni Mwingi wa kupokea toba za waja wake. Maoni ya wataalamu juu ya Surat Annasr:- Sura hii tukufu inaashiria kugomboka kwa Makka. Na sababu khasa iliyo pelekea kugomboka Makka ni Maqureshi walipo vunja mkataba wa amani wa Hudaibiya kwa kuwashambulia kabila ya Khuzaa, ambao walikuwa wana masikilizano na Mtume s.a.w., na wakawasaidia Bani Bakri katika hayo. Yalipo tokea hayo Mtume akaona waliyo yafanya Maqureshi kuvunja mapatano imembidi ende kuigomboa Makka. Basi akakusanya jeshi la nguvu lenye wapiganaji elfu kumi. Akenda mwezi wa Ramadhani katika mwaka wa nane wa Hijra (Desemba mwaka 630 B.K.) Akawazuia watu wake wasipigane ila wakilazimishwa. Na Mwenyezi Mungu alipenda aingie Nabii na jeshi lake Makka bila ya vita. Na kwa hivi akapata ushindi mkubwa kabisa katika taarikhi ya wito wa Kiislamu, bila ya vita. Na Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola ya kwanza duniani bila ya vita na bila ya kumwagwa damu. Na huo ugombozi wa Makka ulikuwa na athari za kufikia mbali kwa pande za Dini na siyasa, kwani ilikuwa ni kuungoa upagani, kuabudu masanamu, katika ngome yake kubwa, kwa kuvunjwa masanamu yaliyo simamishwa katika Al-kaaba, na yakaondolewa mapicha na masanamu yaliyo kuwemo. Na kwa kuingia Makka kwenye boma la Uislamu Nabii s.a.w. aliweza kuzishinda kabila zote zilizo bakia katika Hijazi, ambazo zilizo kuwa zina kani za kijahiliya, kama Hawazan na Thaqif. Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola si juu ya kabila wala nchi bali juu ya Imani, nayo ni Imani ya Kiislamu, na bendera ya Kiislamu
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa
- Siku watakapo sikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya kufufuka.
- Enyi mlio amini! Mnapo nong'ona msinong'one kwa sababu ya mambo ya madhambi, na uadui, na
- Na wanasema walio kufuru: Kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi. Sema: Hakika
- Alif Lam Mym Ra. (A. L. M. R.) Hizi ni Ishara za Kitabu. Na uliyo
- Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa
- Ambao hawatoi Zaka na wanaikataa Akhera.
- Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo watapata neema
- Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu, na uwe miongoni mwa wenye kushukuru.
- Kiovu kweli walicho jiuzia nafsi zao, nacho ni kule kukataa kwao aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nasr with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nasr mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nasr Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers