Surah Yunus aya 21 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً مِّن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُمْ إِذَا لَهُم مَّكْرٌ فِي آيَاتِنَا ۚ قُلِ اللَّهُ أَسْرَعُ مَكْرًا ۚ إِنَّ رُسُلَنَا يَكْتُبُونَ مَا تَمْكُرُونَ﴾
[ يونس: 21]
Na tunapo waonjesha watu rehema baada ya shida waliyo ipata, utawaona wana vitimbi kuzipangia Ishara zetu. Sema: Mwenyezi Mungu ni Mwepesi zaidi wa kupanga. Hakika wajumbe wetu wanayaandika mnayo yapanga.
Surah Yunus in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And when We give the people a taste of mercy after adversity has touched them, at once they conspire against Our verses. Say, "Allah is swifter in strategy." Indeed, Our messengers record that which you conspire
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na tunapo waonjesha watu rehema baada ya shida waliyo ipata, utawaona wana vitimbi kuzipangia Ishara zetu. Sema: Mwenyezi Mungu ni Mwepesi zaidi wa kupanga. Hakika wajumbe wetu wanayaandika mnayo yapanga.
Katika mitindo ya watu ni kuwa pale tunapo waneemesha baada ya kwisha patwa na shida katika nafsi zao, au ahli zao (watu wao), au mali zao, hawamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema anazo waneemesha na kuwaondolea madhara. Bali huyakaabili hayo kwa kukakamia katika kuzikadhibisha na kuzikataa Ishara za Mwenyezi Mungu! Ewe Mtume! Sema: Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kukuhilikini na kukuadhibuni upesi upesi, lau kuwa si hukumu yake tangu hapo kukupeni muhula mpaka siku ya miadi aliyo iweka mwenyewe kwa ilimu yake peke yake. Hakika Wajumbe wetu, Malaika waliyo wakilishwa juu yenu wanaviandika vitimbi mnavyo vipanga, na Yeye Mwenyezi Mungu atakuhisabieni na atakulipeni.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Ameteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabonde yakamiminika maji kwa kadiri yake. Na mafuriko yakachukua mapovu
- Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizo funuliwa.
- Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na
- Na mlipo kutana akakuonyesheni machoni mwenu kuwa wao ni wachache, na akakufanyeni nyinyi ni wachache
- Na lau isinge kuwa watu watakuwa kundi moja tungeli wajaalia wanao mkufuru Rahmani wana nyumba
- Na ambao katika mali yao iko haki maalumu
- Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ana ufalme wa mbingu na ardhi? Nanyi hamna mlinzi wala msaidizi
- Wakasema: Tumemsikia kijana mmoja akiwataja. Anaitwa Ibrahim.
- Wakamkanusha. Basi tukamwokoa, pamoja na walio kuwa naye, katika jahazi. Na tukawafanya wao ndio walio
- Hukuwaona watukufu katika Wana wa Israili baada ya Musa, walipo mwambia Nabii wao: Tuwekee mfalme
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yunus with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yunus mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yunus Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers