Surah Raad aya 31 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَلَوْ أَنَّ قُرْآنًا سُيِّرَتْ بِهِ الْجِبَالُ أَوْ قُطِّعَتْ بِهِ الْأَرْضُ أَوْ كُلِّمَ بِهِ الْمَوْتَىٰ ۗ بَل لِّلَّهِ الْأَمْرُ جَمِيعًا ۗ أَفَلَمْ يَيْأَسِ الَّذِينَ آمَنُوا أَن لَّوْ يَشَاءُ اللَّهُ لَهَدَى النَّاسَ جَمِيعًا ۗ وَلَا يَزَالُ الَّذِينَ كَفَرُوا تُصِيبُهُم بِمَا صَنَعُوا قَارِعَةٌ أَوْ تَحُلُّ قَرِيبًا مِّن دَارِهِمْ حَتَّىٰ يَأْتِيَ وَعْدُ اللَّهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ﴾
[ الرعد: 31]
Na kama ingeli kuwako Qur'ani ndiyo inayo endeshewa milima, na kupasuliwa ardhi, na kusemeshewa wafu, (basi ingeli kuwa Qur'ani hii). Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua walio amini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu ange penda bila ya shaka angeli waongoa watu wote? Wala walio kufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa waliyo yatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ifike ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.
Surah Ar-Rad in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And if there was any qur'an by which the mountains would be removed or the earth would be broken apart or the dead would be made to speak, [it would be this Qur'an], but to Allah belongs the affair entirely. Then have those who believed not accepted that had Allah willed, He would have guided the people, all of them? And those who disbelieve do not cease to be struck, for what they have done, by calamity - or it will descend near their home - until there comes the promise of Allah. Indeed, Allah does not fail in [His] promise.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na kama ingeli kuwako Qurani ndiyo inayo endeshewa milima, na kupasuliwa ardhi, na kusemeshewa wafu, (basi ingeli kuwa Qurani hii). Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua walio amini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu ange penda bila ya shaka angeli waongoa watu wote? Wala walio kufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa waliyo yatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ifike ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.
Wao wanataka muujiza mwingine usio kuwa huu wa Qurani, juu ya ubora wa athari yake, lau kuwa kweli wanaitaka Haki na wanaikubali. Lau kuwa kuna Kitabu cha kusomwa kikaiendesha milima, kikapasua ardhi, au kikawasemeza maiti, basi Kitabu hicho kinge kuwa hii Qurani! Lakini watu hawa wana inda tu. Mwenyezi Mungu peke yake ndiye mwenye amri yote katika miujiza na malipo ya hao wakanyao. Na katika hayo ana uwezo kaamili. Ikiwa hao wamo katika hali hii ya inadi, basi je walio itii Haki hawajakata tamaa bado na kuamini kwa hawa makafiri, na wakajua kwamba kufuru yao ni kuyakataa matakwa ya Mwenyezi Mungu? Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka waongoke watu wote basi wangeli ongoka! Na hakika uwezo wa Mwenyezi Mungu uko dhaahiri mbele yao. Basi haziachi balaa kali kali za kuwateketeza zikiwasibu, au kuwateremkia karibu yao, mpaka itimie ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyo wapa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu havunji miadi yake.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Kina Thamud waliwakanusha Mitume.
- Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana mke wala mwana.
- Amekuharimishieni nyamafu tu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa kwa ajili
- Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu,
- Na iogopeni Siku ambayo mtu hatomfaa mtu kwa lolote, wala hayatakubaliwa kwake maombezi, wala hakitapokewa
- Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima,
- Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na
- Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika
- Na kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun.
- Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanao kejeli.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Raad with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Raad mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Raad Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers