Surah Muhammad aya 4 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿فَإِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا فَضَرْبَ الرِّقَابِ حَتَّىٰ إِذَا أَثْخَنتُمُوهُمْ فَشُدُّوا الْوَثَاقَ فَإِمَّا مَنًّا بَعْدُ وَإِمَّا فِدَاءً حَتَّىٰ تَضَعَ الْحَرْبُ أَوْزَارَهَا ۚ ذَٰلِكَ وَلَوْ يَشَاءُ اللَّهُ لَانتَصَرَ مِنْهُمْ وَلَٰكِن لِّيَبْلُوَ بَعْضَكُم بِبَعْضٍ ۗ وَالَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَلَن يُضِلَّ أَعْمَالَهُمْ﴾
[ محمد: 4]
Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe. Ndio hivyo. Na lau angeli taka Mwenyezi Mungu angeli washinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a'mali zao.
Surah Muhammad in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
So when you meet those who disbelieve [in battle], strike [their] necks until, when you have inflicted slaughter upon them, then secure their bonds, and either [confer] favor afterwards or ransom [them] until the war lays down its burdens. That [is the command]. And if Allah had willed, He could have taken vengeance upon them [Himself], but [He ordered armed struggle] to test some of you by means of others. And those who are killed in the cause of Allah - never will He waste their deeds.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe. Ndio hivyo. Na lau angeli taka Mwenyezi Mungu angeli washinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza amali zao.
Mtapo kutana na walio kufuru katika vita basi wapigeni kwenye shingo zao, mpaka mtakapo wadhoofisha kwa wingi wa kuwauwa, basi tena wafungeni mateka. Tena ama waachilieni wende zao kwa wema na ihsani, baada ya kwisha vita, kwa kuwaachia bila ya fidia, au kwa fidia ya kutoa mali au kubadilishana kwa mateka wa Kiislamu. Inakuwa mmewaachilia kwa badali. Huu ndio uwe mwendo wenu na makafiri mpaka vita vimalizike kabisa. Mwenyezi Mungu anawahukumieni hivyo. Na lau angeli taka bila ya shaka angeli washinda bila ya vita, lakini haya ni ili awajaribu Waumini kwa makafiri kama mtihani ndio ameamrisha Jihadi. Na walio uwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kabisa hatoacha vitendo vyao vipotee. Atawahidi, na azitengeneze nyoyo zao, na awatie katika Pepo aliyo kwisha wajuulisha. Katika Aya hii tukufu zimetajwa -shingo- khasa, kwa sababu kuzipiga hizo ndio njia inayo faa mno kummaliza upesi mwenye kupigwa bila ya kumuadhibu na kumtesa. Kwani imethibiti kwa ilimu kuwa shingo ndiyo kiungo baina ya kichwa na kiwiliwili kizima. Basi ukikatika mshipa wa uti wa mgongo wenye kupeleka hisiya zote, basi viungo vyote muhimu vinapooza. Na ikikatika mishipa ya damu, damu inasita kufika kwenye ubongo. Na zikikatika njia za kupitisha hewa, basi pumzi husita. Na katika hali hizi zote uhai unakatika mara moja.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Nao wakamwacha, wakampa kisogo.
- Na siku atakapo wakusanya wao na hao wanao waabudu, na akasema: Je! Ni nyinyi mlio
- Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa?
- Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe
- Hao ndio wanao sema: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu,
- Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu,
- Na walisema walio kufuru: Haitatufikia Saa (ya Kiyama). Sema: Kwani? Hapana shaka itakufikieni, naapa kwa
- Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu.
- Mna nini? Mbona hamsaidiani?
- NA WANAWAKE wenye waume, isipo kuwa walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Ndiyo Sharia
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Muhammad with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Muhammad mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Muhammad Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers