Surah Anfal aya 41 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ وَاعْلَمُوا أَنَّمَا غَنِمْتُم مِّن شَيْءٍ فَأَنَّ لِلَّهِ خُمُسَهُ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ إِن كُنتُمْ آمَنتُم بِاللَّهِ وَمَا أَنزَلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا يَوْمَ الْفُرْقَانِ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ ۗ وَاللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴾
[ الأنفال: 41]
NA JUENI ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu na tuliyo yateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo, siku yalipo kutana majeshi mawili. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
Surah Al-Anfal in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And know that anything you obtain of war booty - then indeed, for Allah is one fifth of it and for the Messenger and for [his] near relatives and the orphans, the needy, and the [stranded] traveler, if you have believed in Allah and in that which We sent down to Our Servant on the day of criterion - the day when the two armies met. And Allah, over all things, is competent.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
NA JUENI ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu na tuliyo yateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo, siku yalipo kutana majeshi mawili. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
Na enyi Waislamu! Jueni kuwa katika mali ya makafiri mliyo yateka, hukumu yake ni kugawiwa mafungu matano. Fungu moja ni la Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa zake Mtume, na mayatima, nao ni watoto wadogo wa Waislamu waliofiwa na baba zao nao ni mafakiri; na masikini, nao ni wale Waislamu wenye haja; na msafiri, naye ni mwenye kukatikiwa safari yake ya halali. Na yaliyo khusishwa katika hiyo sehemu moja katika tano kuwa ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume hukhusishwa kwa maslaha ya umma kama anavyo pasisha Mtume katika uhai wake, au, baada ya kufa kwake, Imam. Na yaliyo baki katika ile Khumsi watapewa walio kwisha tajwa. Ama sehemu nne nyengine katika ghanima (ngawira), na Aya ikanyamaza kimya juu yake, ni za wale walio pigana. Basi jueni hayo, na myajue ikiwa mmemuamini Mwenyezi Mungu kweli, na mmeziamini Ishara tulizo mteremshia mja wetu, Muhammad, za kumthibitisha na kumsaidia, siku ya Mpambanuo, tulipo pambanua baina ya ukafiri na Imani, nayo ndiyo siku lilipo kutana kundi lenu na kundi la makafiri katika Badri. Na Mwenyezi Mungu Mwenye kudra kubwa juu ya kila kitu aliwapa ushindi Waumini juu ya uchache wao, kuwashinda makafiri juu ya wingi wao.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Walipo wajia Mitume mbele yao na nyuma yao wakawaambia: Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu! Wakasema: Angeli
- Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za
- Basi onjeni kwa vile mlivyo usahau mkutano wa Siku yenu hii. Na Sisi hakika tunakusahauni.
- Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
- Na tulimtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaa'qub. Na tukajaalia katika dhuriya zake Unabii na Kitabu, na
- Hakika wale walio amini, na wakatenda mema, na wakanyenyekea kwa Mola wao Mlezi, hao ndio
- Na akamwona mara nyingine,
- Na neema walizo kuwa wakijistareheshea!
- Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.
- Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, husema: Bali tunafuata tuliyo wakuta nayo baba
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anfal with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anfal mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anfal Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers