Surah Anfal aya 42 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿إِذْ أَنتُم بِالْعُدْوَةِ الدُّنْيَا وَهُم بِالْعُدْوَةِ الْقُصْوَىٰ وَالرَّكْبُ أَسْفَلَ مِنكُمْ ۚ وَلَوْ تَوَاعَدتُّمْ لَاخْتَلَفْتُمْ فِي الْمِيعَادِ ۙ وَلَٰكِن لِّيَقْضِيَ اللَّهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا لِّيَهْلِكَ مَنْ هَلَكَ عَن بَيِّنَةٍ وَيَحْيَىٰ مَنْ حَيَّ عَن بَيِّنَةٍ ۗ وَإِنَّ اللَّهَ لَسَمِيعٌ عَلِيمٌ﴾
[ الأنفال: 42]
Kumbukeni pale mlipo kuwa nyinyi kwenye ng'ambo ya karibu ya bonde, na wao wakawa ng'ambo ya mbali, na msafara ulipo kuwa chini yenu. Na ingeli kuwa mmeagana mngeli khitalifiana katika miadi. Lakini (mkakutana) ili Mwenyezi Mungu atimize jambo lilio kuwa lazima litendeke, kwa sababu aangamie wa kuangamia kwa dalili zilizo dhaahiri, na asalimike wa kusalimika kwa dalili zilizo dhaahiri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.
Surah Al-Anfal in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
[Remember] when you were on the near side of the valley, and they were on the farther side, and the caravan was lower [in position] than you. If you had made an appointment [to meet], you would have missed the appointment. But [it was] so that Allah might accomplish a matter already destined - that those who perished [through disbelief] would perish upon evidence and those who lived [in faith] would live upon evidence; and indeed, Allah is Hearing and Knowing.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Kumbukeni pale mlipo kuwa nyinyi kwenye ngambo ya karibu ya bonde, na wao wakawa ngambo ya mbali, na msafara ulipo kuwa chini yenu. Na ingeli kuwa mmeagana mngeli khitalifiana katika miadi. Lakini (mkakutana) ili Mwenyezi Mungu atimize jambo lilio kuwa lazima litendeke, kwa sababu aangamie wa kuangamia kwa dalili zilizo dhaahiri, na asalimike wa kusalimika kwa dalili zilizo dhaahiri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.
Na kumbukeni mlipo kuwa bondeni ngambo hii ya karibu na Madina, na wao makafiri wako ngambo ile ya mbali, na msafara wenye bidhaa mlio kuwa mnautaka uko karibu zaidi nanyi upande wa baharini. Na lau kuwa mmepeana miadi ya kukutana kwa kupigana basi msinge wafikiana hivyo. Lakini Mwenyezi Mungu kapanga mkutane bila ya miadi, na bila ya kutaka wao, ili apate kutekeleza jambo ambalo katika ujuzi wake limekwisha thibiti litokee tu, wala hapana jenginelo. Jambo lenyewe ni kuwa vitokee vita vitavyo pelekea nyinyi mshinde na wao washindwe. Ipate kuondoka shaka - wateketee wa kuteketea kwa hoja wazi ya kuonekana, nako ni kushindwa makafiri juu ya wingi wao; na wahuike Waumini kwa hoja iliyo wazi, nako ni kushinda kulio toka kwa Mwenyezi Mungu kuwapa Waumini wachache. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na kujua. Haimfichikii kauli wala niya yoyote ya pande zote mbili.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini.
- Basi yule bwana alipoona kanzu yake imechanwa kwa nyuma, alisema: Hakika haya ni katika vitimbi
- Na mnapo adhinia Sala wao wanaichukulia maskhara na mchezo. Hayo ni kwa sababu wao ni
- Wala si mzaha.
- Watakuambia mabedui walio baki nyuma: Yametushughulisha mali yetu na ahali zetu, basi tuombee msamaha. Wanasema
- Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.
- Akasema: Ewe Adam! Waambie majina yake. Basi alipo waambia majina yake alisema: Sikukwambieni kwamba Mimi
- Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo.
- Basi, je! Wanangojea jingine ila kama yaliyo tokea siku za watu walio pita kabla yao?
- Watu wanao mkaribia zaidi Ibrahim ni wale walio mfuata yeye na Nabii huyu na walio
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anfal with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anfal mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anfal Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



