Surah Muminun aya 5 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ﴾
[ المؤمنون: 5]
Na ambao wanazilinda tupu zao,
Surah Al-Muminun in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And they who guard their private parts
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na ambao wanazilinda tupu zao!
Nao wanajihifadhi nafsi zao wasiingiane na wanawake. -Na ambao wanazilinda tupu zao, isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa. Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka.- Aya hizi zinaambatana na Aya nyengine ziliomo katika Suratun Nur zilio anzia: -Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mpigeni kila mmoja wao bakora mia.- Hakika Aya hizi tukufu zilizo tajwa zinaashiria maovu ya katika umma yanayo tokea kwa uzinzi. Ama katika umma ni kuvurugika nasaba ya watoto isijuulikane, ama katika siha ni sehemu mbili. KWANZA ni katika mwili, mfano wa kisonono, tego, AIDS n.k. Kisonono huweza kuzalisha maradhi ya urithi kwa watoto hata huweza kuleta upofu. Ama tego (Syphilis) huenea katika mishipa ya damu na ya hisiya na huweza kuishia wazimu, na pia huenea mpaka kwa vizazi, na huenda mtoto akafa tumboni au akatoka na kilema. Ama maradhi ya AIDS (Ukimwi) hayo ni maafa yasiyo semeka, Mwenyezi Mungu atulinde nayo. PILI ni kuathirika mishipa ya hisiya na akili, kwani uzinzi huweza kuathiri dhamiri ya mtu, na kuadhibika nayo, na hata mwishoe huweza kuingia wazimu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Kisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipo wafikia Mtume wao walimkanusha.
- Na Mtume alikuwa akisema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur'ani ni
- Ambao walifanya jeuri katika nchi?
- Na kipofu na mwenye kuona hawalingani; na walio amini na watendao mema hawalingani na muovu.
- Ama amemzulia Mwenyezi Mungu uwongo, au ana wazimu. Bali wasio amini Akhera wamo adhabuni na
- Mwenye wasaa atoe kadiri ya wasaa wake, na mwenye dhiki atoe katika alicho mpa Mwenyezi
- Na watasema: Je, tutapewa muhula?
- Tuwatupie mawe ya udongo,
- Kisha akamsahilishia njia.
- Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Muminun with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Muminun mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Muminun Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers