Surah Furqan aya 53 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ وَهُوَ الَّذِي مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ هَٰذَا عَذْبٌ فُرَاتٌ وَهَٰذَا مِلْحٌ أُجَاجٌ وَجَعَلَ بَيْنَهُمَا بَرْزَخًا وَحِجْرًا مَّحْجُورًا﴾
[ الفرقان: 53]
Naye ndiye aliye zipeleka bahari mbili, hii tamu mno, na hii ya chumvi chungu. Na akaweka baina yao kinga na kizuizi kizuiacho.
Surah Al-Furqan in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And it is He who has released [simultaneously] the two seas, one fresh and sweet and one salty and bitter, and He placed between them a barrier and prohibiting partition.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Naye ndiye aliye zipeleka bahari mbili, hii tamu mno, na hii ya chumvi chungu. Na akaweka baina yao kinga na kizuizi kizuiacho.
Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziendesha bahari mbili, bahari ya maji matamu na bahari ya maji ya chumvi. Na akafanya njia ya kila moja inakaribiana na nyengine. Na juu ya hivyo maji yao hayachanganyikani. Hiyo ni neema na rehema kwa watu. -Naye ndiye aliye zipeleka bahari mbili, hii tamu mno, na hii ya chumvi chungu. Na akaweka baina yao kinga na kizuizi kizuiacho.- Yamkini Aya hii inaashiria neema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake kwa kuto changanyika maji ya chumvi yanayo penya kutoka baharini kwenye miamba ya karibu na mwambao, na maji matamu yanayo penya kutoka bara, yasichanganyike kwa ukamilifu na hali nayo yanakutana. Matamu yanakuwa yako juu ya maji chumvi kama kwamba baina yao pana kinga kinacho zuia haya yasiingiane na haya, na kizuizi kizuiacho, yaani kizuizi chembamba tusicho weza kukiona. Na haya si tu, bali ipo kanuni madhubuti inayo hukumu makhusiano haya, na inayo yahukumu kwa maslaha ya wanaadamu wanao kaa katika maeneo hayo, na maisha yao yanategemea kuwepo hayo maji matamu. Kwani imethibiti kuwa tabaka ya maji matamu yalioko juu huzidi unene wake kwa mujibu wa kuzidi usawa (level) wa bahari kwa mpango maalumu. Hata inakuwa yawezekana kuhisabu kina cha mwisho cha maji matamu ambayo yamkinika kuyapata. Kwani hiyo ni sawa sawa na kadri ya khitilafu baina ya usawa (level) wa ardhi na usawa wa bahari mara arubaini.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na wanapo kutana na walio amini husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao na mashet'ani
- Sema: Kila mmoja anangoja. Basi ngojeni! Hivi karibuni mtajua nani mwenye njia sawa na nani
- Wanakuuliza khabarai ya miezi. Sema: Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na
- Basi tukawapelekea tufani, na nzige, na chawa, na vyura, na damu, kuwa ni Ishara mbali
- Na kwa usiku unapo lifunika!
- Kwa hakika wale walio kufuru hazitowafaa kitu kwa Mwenyezi Mungu mali zao, wala watoto wao;
- Isipo kuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda.
- Ili watu wa Kitabu wajue kwamba wao hawana uweza wowote juu ya fadhila za Mwenyezi
- Na anaye tenda mema, naye ni Muumini, basi hatakhofu kudhulumiwa wala kupunjwa.
- Basi ameangamia! Vipi alivyo pima!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Furqan with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Furqan mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Furqan Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers