Surah Anam aya 59 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ﴾
[ الأنعام: 59]
Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilioko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinacho bainisha.
Surah Al-Anam in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And with Him are the keys of the unseen; none knows them except Him. And He knows what is on the land and in the sea. Not a leaf falls but that He knows it. And no grain is there within the darknesses of the earth and no moist or dry [thing] but that it is [written] in a clear record.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilioko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinacho bainisha.
Ni Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ujuzi wa milango yote ya vilio ghaibu, visio juulikana na wengine. Hapana Mwenye kukusanya ujuzi wa hivyo ila Yeye, na anao wataka kuwapa baadhi yake. Naye ujuzi wake umekusanya vitu vyote vilioko nchi kavu na vilioko baharini. Wala halidondoki jani, jani lolote lile, ila Yeye analijua, wala haianguki mbegu chini ya ardhi, wala chochote kilicho kinyevu au kikavu, ila Yeye Subhanahu anakijua kwa utimilifu. Kauli hii inafahamisha kuwa kujua mambo ya ghaibu kuko kwa Mwenyezi Mungu, na funguo za hayo ziko kwake tu. Na mambo ya ghaibu ni mafungu mawili: Ghaibu Mutlaq ambayo hayumkini kutambulikana na akili, kama mambo yatakayo mfikia mtu katika mustakbali. Na Ghaib Nisbiy hizi ni siri za ulimwengu na viliomo ndani yake, na kuweza kuvitumia kwa maslaha ya watu. Ujuzi wa hayo huweza kughibu kwa vizazi kadhaa, kisha ukadhihiri.. Na funguo ya hizi pia ziko kwa Mwenyezi Mungu, humwezesha amtakaye katika waja wake wale wanao zama kuusoma ulimwengu. Na katika hayo ni haya ya uvumbuzi ambao tunauona anao ufikilia mwanaadamu kwa kuwezeshwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na
- Hakika wale walio muabudu ndama, itawapata ghadhabu ya Mola wao Mlezi na madhila katika maisha
- Na waambie wale wasio amini: Fanyeni muwezavyo, nasi pia tunafanya.
- Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake,
- Hakika wewe ni miongoni mwa walio tumwa,
- Sema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo
- Kumekushughulisheni kutafuta wingi,
- Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini, akasema: Enyi watu wangu! Wafuateni
- Ewe Nabii! Watakapo kujia wanawake Waumini wanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala
- Hali ya wasio iamini Akhera ni ovu; na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye sifa tukufu. Naye
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anam with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anam mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anam Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers