Surah Maidah aya 6 , Swahili translation of the meaning Ayah.

  1. Arabic
  2. tafsir
  3. mp3
  4. English
Quran in Swahili QUR,ANI TUKUFU na tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili - Ali Muhsen Alberwany & English - Sahih International : Surah Maidah aya 6 in arabic text(The Table).
  
   

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُم مِّنْ حَرَجٍ وَلَٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
[ المائدة: 6]

Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lilio safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.

Surah Al-Maidah in Swahili

Swahili Translation - Al-Barwani

English - Sahih International


O you who have believed, when you rise to [perform] prayer, wash your faces and your forearms to the elbows and wipe over your heads and wash your feet to the ankles. And if you are in a state of janabah, then purify yourselves. But if you are ill or on a journey or one of you comes from the place of relieving himself or you have contacted women and do not find water, then seek clean earth and wipe over your faces and hands with it. Allah does not intend to make difficulty for you, but He intends to purify you and complete His favor upon you that you may be grateful.


Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili


Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Swala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lilio safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.


Enyi Waumini! Mkitaka kuswali nanyi hamna udhu, tawadhini kwa kukosha nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake maji kichwa kizima au baadhi yake. Na mkoshe miguu yenu mpaka vifundoni. Mnapo taka kuswali nanyi mna janaba kwa kuingiliana na wake zenu, basi kogeni mwili mzima. Ikiwa mna maradhi ambayo hayakufaliini kutumia maji, au mpo safarini na ipo taabu ya maji, au mmetoka chooni kukidhi haja, au mmeingiliana (kwa lugha ya Qurani -kugusana-) na wanawake na msipate maji, basi inakupaseni kutayamamu, yaani kujipaka vumbi lilio safi. Na hayo ni kwa kupangusa kwa hilo vumbi nyuso zenu na mikono yenu. Na Mwenyezi Mungu hataki kukudhikini katika hayo anayo kuamrisheni, bali anakupeni sharia za kukusafisheni ndani na nje, ili atimize neema zake juu yenu kwa uwongofu, na kubainisha na kusahilisha, mpate kumshukuru kwa uwongofu wake na kutimilia neema yake kwa kudumisha utiifu kwake. tahara (Usafi) wa Kiislamu una maana mbili: Moja ni kumwelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu moyoni kwa kujiweka tayari kwa hayo, na kufunga azimio kusimama mbele yake na hali ni mwenye nafsi iliyo taahiri, na moyo ulio safi kabisa kwake Yeye tu. Pili ni unadhifu wa dhaahiri kwa udhu. Na katika hayo ni kuvikosha viungo vyote vinavyo weza kuchafuka. Na udhu ni jambo la kufanywa mara kwa mara, na huweza kufika hata kutwa mara tano. Pia kuna kukoga unapo ingiliana na mke, na wakati wa damu ya mwezi na uzazi. Udhu na kukoga ni kuondoa takataka zenye vijidudu vya maradhi, na pia huleta uchangamfu kwa kusisimua damu ya kwenye ngozi, na kupoza mishipa. Na kwa hivyo Mtume s.a.w. aliusia: -Ukihamaki tawadha-.

English Türkçe Indonesia
Русский Français فارسی
تفسير Bengali Urdu

listen to Verse 6 from Maidah


Ayats from Quran in Swahili


Quran Surah in Swahili :

Al-Baqarah Al-'Imran An-Nisa'
Al-Ma'idah Yusuf Ibrahim
Al-Hijr Al-Kahf Maryam
Al-Hajj Al-Qasas Al-'Ankabut
As-Sajdah Ya Sin Ad-Dukhan
Al-Fath Al-Hujurat Qaf
An-Najm Ar-Rahman Al-Waqi'ah
Al-Hashr Al-Mulk Al-Haqqah
Al-Inshiqaq Al-A'la Al-Ghashiyah

Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :

Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Surah Maidah Ahmed El Agamy
Ahmed Al Ajmy
Surah Maidah Bandar Balila
Bandar Balila
Surah Maidah Khalid Al Jalil
Khalid Al Jalil
Surah Maidah Saad Al Ghamdi
Saad Al Ghamdi
Surah Maidah Saud Al Shuraim
Saud Al Shuraim
Surah Maidah Abdul Basit Abdul Samad
Abdul Basit
Surah Maidah Abdul Rashid Sufi
Abdul Rashid Sufi
Surah Maidah Abdullah Basfar
Abdullah Basfar
Surah Maidah Abdullah Awwad Al Juhani
Abdullah Al Juhani
Surah Maidah Fares Abbad
Fares Abbad
Surah Maidah Maher Al Muaiqly
Maher Al Muaiqly
Surah Maidah Muhammad Siddiq Al Minshawi
Al Minshawi
Surah Maidah Al Hosary
Al Hosary
Surah Maidah Al-afasi
Mishari Al-afasi
Surah Maidah Yasser Al Dosari
Yasser Al Dosari


Monday, May 13, 2024

لا تنسنا من دعوة صالحة بظهر الغيب