Surah Hajj aya 78 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَجَاهِدُوا فِي اللَّهِ حَقَّ جِهَادِهِ ۚ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ مِّلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ ۚ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِن قَبْلُ وَفِي هَٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ ۚ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاعْتَصِمُوا بِاللَّهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ ۖ فَنِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ﴾
[ الحج: 78]
Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa.
Surah Al-Hajj in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And strive for Allah with the striving due to Him. He has chosen you and has not placed upon you in the religion any difficulty. [It is] the religion of your father, Abraham. Allah named you "Muslims" before [in former scriptures] and in this [revelation] that the Messenger may be a witness over you and you may be witnesses over the people. So establish prayer and give zakah and hold fast to Allah. He is your protector; and excellent is the protector, and excellent is the helper.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qurani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa.
Na wanieni katika Jihadi ya kunyanyua Neno la Mwenyezi Mungu na kutafuta radhi zake mpaka mwashinde maadui zenu na myashinde matamanio yenu. Kwani Yeye Subhanahu amekukaribisheni kwake, na amekuteueni muinusuru Dini yake, na amekujaalieni muwe Umma wa katikati. Wala hakukulazimisheni katika aliyo kuwekeeni Sharia lolote lenye mashaka juu yenu msilo weza kulichukua. Na amekufanyieni mepesi katika yanayo kuleteeni mashaka, na katika msiyo yaweza amekufanyieni ruhusa namna mbali mbali. Basi ishikeni Dini hii, kwani hii ndiyo Dini ya baba yenu Ibrahim katika misingi yake. Na Yeye Subhanahu ndiye aliye kuiteni Waislamu, (yaani Wanyenyekevu) katika Vitabu vya mbinguni vilivyo tangulia, na pia katika hii Qurani kwa utiifu wenu kwa yale aliyo kutungieni sharia. Basi kueni kama alivyo kuiteni Mwenyezi Mungu ili muwe mwisho wenu mnamshuhudia Mtume kama amekufikishieni ujumbe nanyi mkatenda aliyo kufikishieni, mpate kufanikiwa, na muwe mashahidi kwa kaumu zilizo tangulia kwa yaliyo kuja katika Qurani kwamba Mitume wao nao walifikisha ujumbe. Na ilivyo kuwa Mwenyezi Mungu amekuchagueni nyinyi khasa kuwa ni watiifu kwake, mkashika Swala kwa ukomo wa ukamilifu wake, basi ni waajibu wenu kulipa hayo kwa kumshukuru na kumtii, mshike Swala kwa utimilifu wake, na mwape Zaka wanao stahiki, na mumtegemee Mwenyezi Mungu katika mambo yenu yote, na mchukue kwake msaada, kwani Yeye ndiye Msaidizi wenu na ndiye wa kuwanusuru. Yeye ndiye Mbora wa ulinzi na Mbora wa kunusuru.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- (Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni mwendawazimu.
- Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.
- Hakika Mwenyezi Mungu huwakinga walio amini. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila khaini mwingi wa kukanya
- Alif Lam Raa. Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha.
- Ambaye amekufanyieni ardhi kama tandiko, na akakufanyieni ndani yake njia mpate kuongoka.
- Na itupe fimbo yako! Alipo iona ikitikisika kama nyoka, aligeuka nyuma wala hakungoja. Ewe Musa!
- Sema: Mola wetu Mlezi atatukusanya, kisha atatuhukumu kwa haki; na Yeye ndiye Hakimu Mwenye kujua.
- Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
- Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa.
- Na kama wakigeuka basi Mwenyezi Mungu anawajua waharibifu.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Hajj with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Hajj mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Hajj Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



