Перевод суры Ан-Наба на суахили язык
عَمَّ يَتَسَاءَلُونَ(1) WANAULIZANA nini? |
عَنِ النَّبَإِ الْعَظِيمِ(2) Ile khabari kuu, |
الَّذِي هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ(3) Ambayo kwayo wanakhitalifiana. |
كَلَّا سَيَعْلَمُونَ(4) La! Karibu watakuja jua. |
ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ(5) Tena la! Karibu watakuja jua. |
أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا(6) Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko? |
وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا(7) Na milima kama vigingi? |
وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا(8) Na tukakuumbeni kwa jozi? |
وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا(9) Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko? |
وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا(10) Na tukaufanya usiku ni nguo? |
وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا(11) Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha? |
وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا(12) Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu? |
وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا(13) Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto; |
وَأَنزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا(14) Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni, |
لِّنُخْرِجَ بِهِ حَبًّا وَنَبَاتًا(15) Ili tutoe kwayo nafaka na mimea, |
وَجَنَّاتٍ أَلْفَافًا(16) Na mabustani yenye miti iliyo kamatana. |
إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ كَانَ مِيقَاتًا(17) Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake, |
يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا(18) Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi, |
وَفُتِحَتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ أَبْوَابًا(19) Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango, |
وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا(20) Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi. |
إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا(21) Hakika Jahannamu inangojea! |
لِّلطَّاغِينَ مَآبًا(22) Kwa walio asi ndio makaazi yao, |
لَّابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا(23) Wakae humo karne baada ya karne, |
لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا(24) Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji, |
إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا(25) Ila maji yamoto sana na usaha, |
جَزَاءً وِفَاقًا(26) Ndio jaza muwafaka. |
إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا(27) Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu. |
وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا(28) Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu. |
وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا(29) Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika. |
فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا(30) Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu! |
إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا(31) Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu, |
حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا(32) Mabustani na mizabibu, |
وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا(33) Na wake walio lingana nao, |
وَكَأْسًا دِهَاقًا(34) Na bilauri zilizo jaa, |
لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا(35) Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo - |
جَزَاءً مِّن رَّبِّكَ عَطَاءً حِسَابًا(36) Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha. |
رَّبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الرَّحْمَٰنِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا(37) Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake! |
يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّا ۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَٰنُ وَقَالَ صَوَابًا(38) Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu. |
ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الْحَقُّ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ مَآبًا(39) Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi. |
إِنَّا أَنذَرْنَاكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنظُرُ الْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ الْكَافِرُ يَا لَيْتَنِي كُنتُ تُرَابًا(40) Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo! |
Больше сур в суахили:
Скачать суру An-Naba с голосом самых известных рекитаторов Корана:
Сура An-Naba mp3: выберите рекитатора, чтобы прослушать и скачать главу An-Naba полностью в высоком качестве
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Помолитесь за нас хорошей молитвой