Surah An Naba aya 9 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا﴾
[ النبأ: 9]
Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko?
Surah An-Naba in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And made your sleep [a means for] rest
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko?
Na tukafanya kulala kwenu ni mapumziko ya machofu ya kazi? Kulala usingizi ni kusita nishati ya sehemu ya ubongo yenye kutambua na kuwa macho. Yaani gamba la ubongo, au kupunguka nishati yake kwa wingi, ukilinganisha na daraja za nishati ya sehemu za viungo vilio baki. Na kwa hivyo kunapunguka nguvu na joto la mwili, tena mwili hapo wakati wa usingizi hupata kutua na kupumzika baada ya kuhangaika viungo au akili au vyote viwili. Basi kazi za kimwili zote hupunguka isipo kuwa kazi za kusaga chakula, na kupitisha mkojo katika mafigo, na kutoka majasho katika ngozi, kwani yakisita hayo hupatikana madhara juu ya maisha ya mtu. Ama kuvuta pumzi huko nako hupunguka, na huwa ni kwa ndani zaidi, na huwa kwa kifua zaidi kuliko kwa tumbo. Na mpigo wa mishipa hupungua kasi kwa kunavyo tokana na moyo, na hudhoofika mkazano wa musulo (muscular tension), na kwa hivyo huwa taabu kupata harakati za kinyume. Na yote haya ni ili binaadamu apate kupumzika wakati wa kulala.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
- ALIF LAM MYM 'SAAD
- Kisha tukawazamisha wale wengine.
- Au wanayo sehemu ya utawala? Basi hapo wasingewapa watu hata tundu ya kokwa ya tende.
- Na alipo kwisha watengenezea mahitaji yao akakitia kikopo cha kunywea maji katika mzigo wa nduguye
- Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas,
- Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Hayo ndiyo aliyo wabashiria Mwenyezi Mungu waja wake walio amini na wakatenda mema. Sema: Sikuombeni
- Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika
- Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah An Naba with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah An Naba mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter An Naba Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers