Surah Maidah aya 103 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿مَا جَعَلَ اللَّهُ مِن بَحِيرَةٍ وَلَا سَائِبَةٍ وَلَا وَصِيلَةٍ وَلَا حَامٍ ۙ وَلَٰكِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ ۖ وَأَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ﴾
[ المائدة: 103]
Mwenyezi Mungu hakujaalia uharamu wowote juu ya "Bahira" wala "Saiba" wala "Wasila" wala "Hami". Lakini walio kufuru humzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na wengi wao hawatumii akili.
Surah Al-Maidah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Allah has not appointed [such innovations as] bahirah or sa'ibah or wasilah or ham. But those who disbelieve invent falsehood about Allah, and most of them do not reason.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Mwenyezi Mungu hakujaalia uharamu wowote juu ya -Bahira- wala -Saiba- wala -Wasila- wala -Hami-. Lakini walio kufuru humzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na wengi wao hawatumii akili.
Mwenyezi Mungu hakukupeni ruhusa kuharimisha kitu alicho kuhalalishieni, na kwa hivyo mkenda mkawapasua ngamia masikio yao, na mkajizuia kuwatumia mkawaita -Bahira- mkawawacha kwa kuwekea nadhiri, na mkawaita -Saiba-; na mkaharimisha kula kondoo dume, na mkawatoa kuwa tunza kwa masanamu; na hata kondoo akizaa dume na jike mkamwita -Wasila-, na mkakataa kumchinja dume lake. Wala Mwenyezi Mungu hakukufanyieni sharia ya kukuharimishieni msimtumie ngamia dume baada wakisha zalikana kutokana naye matumbo kumi, naye mkamwita -Hami-! Mwenyezi Mungu hakukutungieni sharia yoyote ya namna hiyo. Lakini walio kufuru wanazua uwongo na wanamsingizia Mwenyezi Mungu. Na wengi wao hawatumii akili. Wakati wa Jahiliya, kabla ya Uislamu, Waarabu wakijiharimshia wenyewe asiyo yaharimisha Mwenyezi Mungu. Katika hizo ni kuwa:- 1. Ngamia akizaa mara tano na mtoto wa mwisho akawa dume, basi wakimpasua sikio lake na wakaharimisha kumpanda, na akawa haijuzu kumfukuza kwenye kunywa maji au kula machunga. Na wakimwita: -Bahira-, yaani aliyepasuliwa sikio. 2. Ilikuwa mtu husema: Nikirejea safarini, au nikipona maradhi yangu, basi ngamia wangu ni -Saiba-, yaani aliye achwa, na anakuwa kama -Bahira-. 3. Na walikuwa kondoo akizaa jike humfanya huyo mtoto ni wao, na akizaa dume humfanya ni wa miungu yao; na akizaa dume na jike basi hawamtoi mhanga huyo dume tena kwa miungu yao, na humwita huyo kondoo jike: -WAsila-, yaani amemuwasilia nduguye dume. 4. Na pia walikuwa akitokana na fahali mizao kumi basi husema mgongo wake umehamika,yaani umehifadhika, na wakamwita -Hami-. Huwa basi hapandwi, wala hatwikiwi mizigo.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na hapo kabla yake waliikataa, na wakiyatupilia mbali maneno ya ghaibu kutoka mahali mbali.
- Sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Muumba mbingu na ardhi! Mjuzi wa yasiyo onekana na yanayo onekana!
- Na mtu akiguswa na shida hutuomba naye kaegesha ubavu, au kakaa, au kasimama. Lakini tukimwondoshea
- SOMA uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu.
- Je! Wanaaminisha kuwa haitowajia adhabu ya Mwenyezi Mungu ya kuwagubika, au haitawafikia Saa ya Kiyama
- Hakika wale walio amini na wakahama na wakapigania Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao
- Akasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba?
- Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo.
- Na vyake Yeye vilivyo mbinguni na katika ardhi. Vyote vinamt'ii Yeye.
- Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers