Surah Hud aya 110 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ﴾
[ هود: 110]
Na kwa yakini tulimpa Musa Kitabu; zikazuka khitilafu ndani yake. Na lau kuwa si neno lilio kwisha tangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka ingeli hukumiwa baina yao. Na hakika wao wamo katika shaka juu yake inayo wahangaisha.
Surah Hud in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And We had certainly given Moses the Scripture, but it came under disagreement. And if not for a word that preceded from your Lord, it would have been judged between them. And indeed they are, concerning the Qur'an, in disquieting doubt.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na kwa yakini tulimpa Musa Kitabu; zikazuka khitilafu ndani yake. Na lau kuwa si neno lilio kwisha tangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka ingeli hukumiwa baina yao. Na hakika wao wamo katika shaka juu yake inayo wahangaisha.
Na Sisi tunakuhakikishia, ewe Nabii, kwamba tulimpa Musa Taurati. Na watu wake baada yake wakakhitalifiana katika tafsiri yake na maana yake, kwa kufuata pumbao lao na matamanio yao. Kila mmoja wao anataka kuielekeza ifuate matamanio yake. Wakafarikiana makundi mbali mbali. Wengi wao wakajitenga na Haki iliyo wajia. Na lau kuwa ahadi ya Mwenyezi Mungu haikutangulia kuwa itaakhirishwa adhabu yao mpaka Siku ya Kiyama, ingeli wateremkia katika hii dunia yao hukumu ya Mwenyezi Mungu wakateketezwa wapotovu na wakaokoka walio na haki, kama yalivyo washukia wengineo, walio jiwa na ujumbe wakakhitalifiana katika kuufahamu baadae, na wakaugeuza, hata ikawa ni uzito kuifahamu kweli. Na hawa walio irithi Taurati wanababaika hawaijui kweli iko wapi!
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu wa haki. Na kipo kitu gani baada
- Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
- Na siku watakapo letwa walio kufuru kwenye Moto wataambiwa: Nyinyi mlitwaa vitu vyenu vizuri katika
- Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea.
- Kwa nini usiwepo mji mmoja ukaamini na Imani yake ikawafaa - isipo kuwa kaumu Yunus?
- Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote.
- Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu
- Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote
- Na Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wako wanao wapanda, na baadhi yao wanawala.
- Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Hud with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Hud mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Hud Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



