Surah Baqarah aya 114 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَا ۚ أُولَٰئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَا إِلَّا خَائِفِينَ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴾
[ البقرة: 114]
Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye zuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake na akajitahidi kuiharibu? Watu hao haitawafalia kuingia humo ila nao wanaogopa. Duniani watapata hizaya na Akhera watapata adhabu kubwa.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And who are more unjust than those who prevent the name of Allah from being mentioned in His mosques and strive toward their destruction. It is not for them to enter them except in fear. For them in this world is disgrace, and they will have in the Hereafter a great punishment.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye zuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake na akajitahidi kuiharibu? Watu hao haitawafalia kuingia humo ila nao wanaogopa. Duniani watapata hizaya na Akhera watapata adhabu kubwa.
Katika yanayo dhihirisha uadui wa wao kwa wao na uadui wao wote kwa Waislamu, ni kule baadhi ya mataifa yao yalivyo kuwa yakiharibu pahala mwa ibada ya mataifa mengineo, na vile wale washirikina walivyo kuwa wakiwazuia Waislamu wasiingie Msikiti Mtakatifu wa Makka. Na hapana kabisa mwenye kudhulumu zaidi kuliko azuiaye asitajwe Mwenyezi Mungu katika pahala pa ibada, na akafanya juhudi kutaka kupaharibu. Watu hao watapata hizaya duniani, na Akhera watapata adhabu kubwa. Haiwafalii wao kufanya ukhalifu kama huu muovu, bali iwapasavyo ni kulinda utakatifu wa pahala pa ibada, wala wasiingie humo ila kwa unyenyekevu na kukhofu, wala wasizuilie kutajwa jina la Mwenyezi Mungu ndani yake. (Na ufisadi kama huu, bali ni mkubwa zaidi, ni wa wale wanao ghusubu (kuiba) mali za wakfu ya misikiti.)
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na siri zote za katika mbingu na ardhi ziko kwa Mwenyezi Mungu. Wala halikuwa jambo
- Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye husamehe yasiyo kuwa hayo kwa amtakaye.
- Na waepushe na maovu; kwani umwepushaye maovu siku hiyo, hakika umemrehemu; na huko ndiko kufuzu
- Na siku hiyo tutawaacha wakisongana wao kwa wao. Na baragumu litapulizwa, na wote watakusanywa pamoja.
- Basi tukamwitikia, na tukamwondolea madhara aliyo kuwa nayo, na tukampa watu wake na mfano wao
- Na kwa wanao toa kwa upole,
- Isipo kuwa njia ya Jahannamu. Humo watadumu milele. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.
- Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo.
- Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
- Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers