Surah Araf aya 142 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ وَوَاعَدْنَا مُوسَىٰ ثَلَاثِينَ لَيْلَةً وَأَتْمَمْنَاهَا بِعَشْرٍ فَتَمَّ مِيقَاتُ رَبِّهِ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ۚ وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَارُونَ اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي وَأَصْلِحْ وَلَا تَتَّبِعْ سَبِيلَ الْمُفْسِدِينَ﴾
[ الأعراف: 142]
Tulimuahidi Musa masiku thalathini na tukayatimiza kwa kumi; ikatimia miadi ya Mola wake Mlezi masiku arubaini. Na Musa akamwambia nduguye Haarun: Shika mahala pangu kwa watu wangu na utengeneze wala usifuate njia ya waharibifu.
Surah Al-Araf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And We made an appointment with Moses for thirty nights and perfected them by [the addition of] ten; so the term of his Lord was completed as forty nights. And Moses said to his brother Aaron, "Take my place among my people, do right [by them], and do not follow the way of the corrupters."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Tulimuahidi Musa masiku thalathini na tukayatimiza kwa kumi; ikatimia miadi ya Mola wake Mlezi masiku arubaini. Na Musa akamwambia nduguye Haarun: Shika mahala pangu kwa watu wangu na utengeneze wala usifuate njia ya waharibifu.
Tulimuahidi Musa tutazungumza naye na tutampa Taurati baada ya kutimia masiku (wingi wa -usiku-) thalathini ya yeye kuabudu. Na tukauongeza muda huo kwa masiku kumi, kutimiza ibada. Yakawa masiku arubaini. Musa akamwambia nduguye Haarun alipo kuwa anakwenda kuzungumza na Mwenyezi Mungu: Kuwa badala yangu kwa hawa watu wangu. Na watengenezee mambo yao yanayo hitajia kutengenezwa. Na tahadhari na kufuata njia ya mafisadi. (Angalia: Kwa Kiswahili safi, -Masiku- ni wingi wa -Usiku-. Ama wingi wa -Siku- ni -Siku- vile vile kama ilivyo katika aghlabu ya maneno mengine yanayo anzia -S-, kama Saa, Sanda, Sahani, Sabuni, Safari, Sufuria n.k.)
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hakika ilikuwapo Ishara kwa (watu wa nchi ya) Sabaa katika maskani yao - bustani mbili,
- Shetani amewatawala na akawasahaulisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hao ndio kundi la Shetani. Kweli hakika kundi
- Qaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu!
- Wala msiwe kama wale walio msahau Mwenyezi Mungu, na Yeye akawasahaulisha nafsi zao. Hao ndio
- Enyi mlio amini! Chukueni hadhari yenu! Na mtoke kwa vikosi au tokeni nyote pamoja!
- Wanakuhimiza waletewe adhabu kwa haraka, na hali Jahannamu kwa hakika imewazunguka makafiri!
- Ama wao wamo katika shaka ya kukutana na Mola wao Mlezi! Ama hakika Yeye amekizunguka
- Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?
- Sisi tunajua vyema kabisa sababu wanayo sikilizia wanapo kusikiliza, na wanapo nong'ona. Wanapo sema hao
- Kisha hakika Mola wako Mlezi, kwa wale walio hama makwao baada ya kuteswa, kisha wakapigania
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Araf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Araf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Araf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



