Surah Yunus aya 3 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِن بَعْدِ إِذْنِهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴾
[ يونس: 3]
Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, na ametawala kwenye ufalme wake, anaendesha mambo yote. Hapana mwombezi ila baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je! Hamkumbuki?
Surah Yunus in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Indeed, your Lord is Allah, who created the heavens and the earth in six days and then established Himself above the Throne, arranging the matter [of His creation]. There is no intercessor except after His permission. That is Allah, your Lord, so worship Him. Then will you not remember?
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, na ametawala kwenye ufalme wake, anaendesha mambo yote. Hapana mwombezi ila baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je! Hamkumbuki?
Enyi watu! Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake katika siku sita ambazo kipimo chake hakijui ila Mwenyezi Mungu. Akatandaza utukufu wa utawala wake, peke yake, na akayapanga mambo yote ya viumbe vyake. Basi hapana yeyote mwenye chochote pamoja na utawala wa Mwenyezi Mungu. Wala hawezi yeyote katika viumbe vyake hata kumwombea mtu isipo kuwa kwa ruhusa yake. Huyo, basi, ndiye Mwenyezi Mungu Muumba, huyo ndiye Mola wenu Mlezi, na ndiye Mlinzi wa neema zenu. Basi muabuduni Yeye peke yake, na msadikini Mtume wake, na kiaminini Kitabu chake. Juu yenu kukumbuka neema za Mwenyezi Mungu, na zingatieni Ishara zake zinazo thibitisha Upweke wake. Mwenyezi Mungu ameumba viumbe vyote kwa vipindi sita, na vipindi hivi ni viwango vya mamilioni ya makarne na makarne. Na hivyo ndivyo vinavyo itwa Siku Sita. Na katika kila nguzo za ulimwengu zipo Ishara wazi zilizo zagaa za kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Miongoni mwa hizi, ni hivi kufanywa jua na mwezi na nyota kunyenyekea kwa faida ya binaadamu. Na kadhaalika kupishana zamu usiku na mchana, na kuwa mchana unaingilia kiza cha mbingu. Na umetajwa usiku mbele kwa kuwa kiza ndio asli. Ama mchana umezuka kwa kuathirika kwa mwangaza wa jua katika anga la ardhi, ambayo hiyo ardhi inazunguka wenyewe kwa wenyewe kama pia ili ipate mwangaza wa jua, mara upande huu na mara upande huu
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Kwa hivyo Mwenyezi Mungu anawaadhibu wanaafiki wanaume, na wanaafiki wanawake, na washirikina wanaume, na washirikina
- Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?
- Wewe huna lako jambo katika haya - ama atawahurumia au atawaadhibu, kwani wao ni madhaalimu.
- Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume.
- Na wasipo kuitikieni, basi jueni ya kwamba (hii Qur'ani) imeteremshwa kwa ujuzi wa Mwenyezi Mungu,
- Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je, hawaoni ya kwamba
- Na tungeli penda tungeli yafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wange ionaje?
- Shika Sala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur'ani ya al fajiri. Hakika
- Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki?
- Mnatumai watakuaminini na hali baadhi yao walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu, kisha wakayabadili baada
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yunus with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yunus mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yunus Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



