Surah Kahf aya 16 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَإِذِ اعْتَزَلْتُمُوهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّهَ فَأْوُوا إِلَى الْكَهْفِ يَنشُرْ لَكُمْ رَبُّكُم مِّن رَّحْمَتِهِ وَيُهَيِّئْ لَكُم مِّنْ أَمْرِكُم مِّرْفَقًا﴾
[ الكهف: 16]
Na mkijitenga nao na vile wanavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu, basi kimbilieni pangoni, akufungulieni Mola wenu Mlezi rehema yake, na akutengenezeeni ya kukufaeni katika mambo yenu.
Surah Al-Kahf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
[The youths said to one another], "And when you have withdrawn from them and that which they worship other than Allah, retreat to the cave. Your Lord will spread out for you of His mercy and will prepare for you from your affair facility."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na mkijitenga nao na vile wanavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu, basi kimbilieni pangoni, akufungulieni Mola wenu Mlezi rehema yake, na akutengenezeeni ya kukufaeni katika mambo yenu.
Na wakaambiana wao kwa wao: Maadamu sisi tumejitenga nao hao katika ukafiri wao na ushirikina wao, basi kimbilieni pangoni mlinde Dini yenu. Mola wenu Mlezi atakukunjulieni maghfira yake, na atakusahilishieni mambo yenu kwa njia za kukufaeni katika maisha yenu. Haijuulikani kwa hakika ni nani hao Ahlil Kahf, wala zama zao, wala hilo pango lipo wapi walilo kimbilia hao vijana. Pamoja na hayo hapana ubaya kuchunguza, huenda pakapatikana mwangaza japo kidogo juu yake. Ilivyo kuwa Qurani Tukufu imetaja kuwa hao walikuwa ni vijana walio muamini Mola wao Mlezi basi hapana budi kuwa wao na watu wao waliteswa kwa sababu ya Dini, hata wakaona hao vijana wakimbilie pangoni kujificha. Na Taarikhi ya zamani inataja kuwa yalikuwako mateso ya dini katika nchi za Mashariki ya kale yaliyo tokea nyakati mbali mbali. Tutataja katika yafuatayo mateso mawili huenda moja wapo likaelekea na kisa hichi:- Ya kwanza yalitokea zama za mfalme wa Kisaluki, Antiokhus IV, aliye itwa kwa jina la kupanga Nabivanis (kiasi ya 176-84 K.K.). Huyo alipo shika ufalme wa Shamu, na akawa amemili mno kwenye ustaarabu wa Kigiriki na ilimu zake, aliwalazimisha Mayahudi wa Palistina, nayo ilikuwa chini ya Shamu tangu mwaka 194 K.K. washike dini ya Kigiriki, na akavunja sharia zao, na akanajisi Hekalu lao kwa kuweka humo sanamu la Zeus, mungu mkuu wa Magiriki, juu ya madhibahu (kibulani), na kumtolea mihanga ya nguruwe humo. Tena huyo mfalme aliteketeza kwa moto nakla za Taurati zote alizo zipata. Kwa mwangaza huu yaonekana kuwa hawa vijana walikuwa ni Mayahudi, na kwao ni popote katika Palastina, au khasa ni katika Yerusalemu. Na ikawa wakaamka mnamo mwaka 126 B.K. zama za utawala wa Warumi wa Mashariki. Yaani kabla ya kuzaliwa Mtume Muhammad s.a.w. (nako kulikuwa kiasi mwaka 571 B.K.) kwa kiasi ya miaka mia nne na arubaini na tano takriban. Ama mateso ya pili yalitokea zama za Mfalme wa Ufalme wa Kirumi, Hadriatus (117-138). Mfalme huyu aliwatenda Mayahudi kama alivyo watendea Antiokhus tuliye kwisha mtaja sawa sawa. Matokeo ya hayo ni kuwa Mayahudi walitangaza uasi dhidi ya utawala wa Kirumi mwaka 132. Wakawafukuza askari wa ulinzi wa Kirumi, wakaiteka Yerusalemu, na wakatoa sarafu yao ya makumbusho ya ugombozi wa Mji Mtakatifu. Wakashika khatamu za utawala kwa muda wa miaka mitatu. Mwishoni Hadriatus na jeshi lake wakagutuka, wakaushinda uasi, na wakairudisha Palastina chini ya utiifu, na wakairudisha Yerusalemu, na wakauvunjilia mbali uwananchi wa Kiyahudi kabisa. Viongozi wa Mayahudi wakauwawa na Mayahudi wakauzwa sokoni kuwa watumwa. Matokeo ya hayo ni kuwa mambo yote ya Kiyahudi aliyapiga marfuku Hadriatus na akapiga marfuku mafunzo ya Kiyahudi na sharia zao. Kwa mujibu wa mwangaza huu wa taarikhi yaonekana kuwa vijana hawa walikuwa ni Mayahudi, na pahala pao ni popote katika Mashariki ya kale, au katika Yerusalemu yenyewe. Yaonekana kuwa waliamshwa mnamo mwaka 435 B.K., yaani kabla ya kuzaliwa Mtume wetu s.a.w. kwa miaka mia na thalathini. Yaonekana kuwa yale mateso ya mwanzo yameelekeana zaidi na kisa hichi cha Watu wa Pangoni, kwa sababu yalikuwa ni ya shida zaidi. Ama mateso ya Kikristo hayaelekeani na kuzaliwa kwa Mtume s.a.w.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa.
- Basi aliwachezea watu wake, na wakamt'ii. Kwa hakika hao walikuwa watu wapotovu.
- Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano!
- Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake,
- Basi kwa haya waite! Nawe simama sawa sawa kama ulivyo amrishwa, wala usiyafuate matamanio yao.
- Na akalifanya jua na mwezi kwa manufaa yenu daima dawamu, na akaufanya usiku na mchana
- Ati wanasema: Amemzulia Mwenyezi Mungu uwongo? Mwenyezi Mungu akipenda atapiga muhuri juu ya moyo wako.
- Yeye ndiye aliye kuumbeni katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili
- Lakini walio mcha Mola wao Mlezi watapata ghorofa zilizo jengwa juu ya ghorofa; chini yake
- Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Kahf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Kahf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Kahf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers